Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Miezi ya karibuni maeneo mengi yatakutwa na hali ya baridi au mvua, na kwa sasa kuna baadhi ya maeneo mvua inanyesha. Na kawaida hali ya mvua au baridi huwa ni baraka kwa wapendanao; kwa wale ambao tunakuwa hatuna wapenzi, huwa tunaishia kula mahindi ya kuchoma, kunywa kahawa, chai ya tangawizi, pamoja na kuvaa makoti, huku tukiwa tumejikunyata kwa kukunja ngumi.
Kipindi hiki kupata penzi jipya huwa ni ngumu sana, ukilinganisha na kipindi cha joto; kwa sababu kipindi hiki cha mvua/baridi kila mmoja huwa anapambana kivyake kulinda joto lake.
Kwa hali hiyo tunawashauri mliopo kwenye mahusiano, kipindi hiki sio cha kutoa talaka wala kuvunja uhusiano; vinginevyo mje mjumuike na sisi huku kwa kula mahindi ya kuchoma, kunywa kahawa, kujikunyata kwa kukunja ngumi n.k