Kipindupindu chaitesa Wilaya ya Tanganyika - Katavi, waripotiwa Wagonjwa 441, Sita wafariki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-11-19 at 14.24.26_824b9642.jpg

Katavi: Hali ya Ugonjwa wa Kipindupindu kufikia Novemba 2024

Wagonjwa waliojitokeza - 441
Walioruhusiwa kutoka Hospitali – 419
Waliopoteza Maisha – 6

Mgawanyiko wa Wagonjwa hao wa Kipindupindu
Wanaume – 235
Wanawake - 206

Umri
Miaka 15+ : 187
Miaka 5 - 15: 150
Miaka 1-4: 92
Chini ya Mwaka 1: 12

Maeneo
Ikola - 245
Isemvula 67
Kapalamsenga 10
Karema 13
Kalya 5

Chanzo: Ofisi ya Katibu Tarafa

Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu husasani Tarafa ya Karema, Wilaya ya Tanganyika imefikia jumla ya wagonjwa 441 huku vifo 6 tayari vimerekodiwa kutokea.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Novemba 18, 2024, Albert Msovela ameiambia (Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Katavi) RCC kuwa kipindupindu kipo na Wagonjwa walioathirika zaidi ni Wanawaume ambao ni Wagonjwa 235 huku Wanawake wagonjwa 206 tofauti kwa idadi ya wagonjwa 29.

Msovela akitoa ripoti hiyo kwenye Kikao cha 23 cha RCC, ametoa mgawanyo wa wathirika kiumri ambapo kwa watu wa miaka 15 na kuendelea idadi yao imeongezeka na kufikia wagonjwa 187.

Kwa watoto wa umri wa miaka 5 hadi 15 idadi ya wagojwa ni 150, Watoto wa umri wa mwaka 1 hadi 4 ni 92 na watoto chini ya mwaka mmoja ni wagonjwa 12 ikiwa katika maeneo yaliyo athirika zaidi ni eneo la Ikola, Isengula, Kapalamsenga, Karema na Kalya.

Katibu Tawala huyo ametaja sababu zinazochagia kuendelea kwa mlipuko wa kipindupindu na zinapaswa kutatuliwa kwa haraka ni pamoja na maji yanayotoka katika vyanzo vilivyopo pia kutokutibiwa kwa kutumia chlorine hivyo jamii kutokuwa na uhakika wa maji safi na salama pamoja na kuanzishwa kwa vijiji visivyokuwa na miundombinu ya maji na vyoo.

“Hatua za mapambano dhidi ya kipindupindu zimekuwa zikilegalega kutokana na ukosefu wa bajeti ya utekelezaji pamoja mwitikio hafifu wa jamii kwenye mapambano ya ugonjwa huo,” amesema Msovela.
WhatsApp Image 2024-11-19 at 14.36.30_e35938c7.jpg

WhatsApp Image 2024-11-19 at 14.36.58_277fbc30.jpg
 
Ccm mbere kwa mbere
 
Mh kama janga hili limeikumba Katavi sioni Sumbawanga kuponyeka kwake maana vyanzo vya maji na aina ya mazingira vinafanana sana.
 
Jenga na tumia choo Bora, kunywa maji salama( chemsha/water guard), nawa mikono Kwa maji na sabuni kabla ya kula na baada ya kutoka chooni. Watanzania vichwa vigumu. Unaenda shamba unakunywa maji ya mto, madimbwi huchemshi unatarajia nn, kunya chooni husikii ila kunya kwenye mito, vichaka unategemea nn
 
Vifo vikizidi, tutasema ni mipango ya shetani dhidi ya serikali.

Manabii, mitume, mashehe, mapadre na waganga wataitwa kuiombea nchi.

Lakini cha ajabu pesa ambazo zingeweza kutumika kwenye primary prevention ya ugonjwa.
 
Back
Top Bottom