Kipindupindu kinatupigisha kwata, je Corona tutaiweza?

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Posts
3,766
Reaction score
4,048
Nimejaribu kufikiria sana juu ya huu ugonjwa corona ukiingia hapa Tanzania matokeoyake yatakuwaje:

1: Ni kama serikali haijalichukulia uzito wa kutosha hili tatizo, kwani njia za kujikinga bado zina utata mkubwa, hasa sehemu za mipakani (Njia zitumikazo kuingia nchini) ulinzi na upimaji haujatiliwa mkazo.

2: Matamko yanayotolewa na viongozi waliopewa dhamana ni ya kisiasa zaidi

3: Kinga ni bora kuliko tiba, sijui serikali imejipangaje kuzuia hili janga na kama wameshaandaa/tafuta vifaa saidizi vya kujikinga, pia kutoa elimu kwa wananchi kila kijiji/kitomngoji, achilia mbali elimu inayotolewa kweny vyombo vya habari - kwani si wote wenye fursa ya kuwa na hivyo vyombo.

NB:
Kipindupindu kikianza huwa kinasumbua sana na watu wengi upoteza maisha, sasa najiuliza hii corona itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…