KERO Kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinaua ni hatari! Mbona Serikali haiweki wazi 'status' ipoje?

KERO Kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinaua ni hatari! Mbona Serikali haiweki wazi 'status' ipoje?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu, nimesikia na kuona ugonjwa wa kipindupindu kushamiri wakati au majira haya ya kiangazi.

Hahahahahahahaha, kwanza inachekesha, lakini pia inahuzunisha, kwani watu wanakufa kweli kweli ingawa ni kimya kimya.

Iko hivi sasa, sikilizeni.

Mkoa wa Simiyu, ni moja ya mkoa ambao kipindi cha masika mwaka huu, wakati wa zile mvua nyingi, ulikumbukwa na ugonjwa au mlipuko wa kipindupindu.

Ugonjwa huu pia uliibuka katika mikoa ya Shinyanga, Mara, Mwanza, Kigoma, katavi, na mikoa mingi nchini, lkn baada ya zile mvua na kuanza msimu wa kiangazi ugonjwa ukatokomea.

Sasa cha ajabu na kushangaza, KIPINDU PINDU, Kimeisha kwenye mikoa mingine lakini Mkoani Simiyu, KIPINDU PINDU kimeganda na kuanza kumeshamiri vibaya sana.

Watu wanakufa, wengi wanapona, ni mamia ya watu ambao wamepata ugonjwa huu mpaka sasa, kwenye kiangazi kama hiki, kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinalipuka kama bomu, kimeua sana.

Kinachoshangaza zaidi, katika mkoa huo kuna Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya Habari, hakuna aliyetangaza, hakuna aliyeripoti ugonjwa huu wala chombo chochote cha habari ambacho kimeripoti ugonjwa huu.

Siyo waandishi tu, hakuna hata kiongozi yeyote wa serikali ambaye ametangaza uwepo wa hili janga ndani ya mkoa, wote wamekaa kimya na ugonjwa unaendelea kuua watu.

Kila siku watu wanakufa na huu ugonjwa, na taarifa zinasema ugonjwa umeshamiri Wilaya za Meatu, Itilima na Bariadi, na katika Wilaya ya Bariadi cha kuchekesha za ugonjwa umeshamiri na unaua Mjini, yaani Halmashauri ya Mji Bariadi.

Mpaka sasa mamia ya wananchi wa mkoa huu, wamekumbwa na ugonjwa huu kwenye hizo Wilaya na baadhi wamekufa, taarifa ambazo nazipata kila siku watu wanakufa kwa ugonjwa huu.

Juzi angalau nimena video ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu simjui jina, akieleza huo ugonjwa, na hiyo video ilikuja baada ya kutokea tafurani katika Wilaya hiyo, watu walilalamika kukamatwa na kutozwa faini kwa wale ambao walikutwa hawana vyoo.

Sasa kwenye hiyo taarifa Mkuu huyo wa Wilaya alisema baadhi ya watu wamekufa kwa ugonjwa huo, na wengine zaidi ya 60 wanaendelea kupatiwa matibabu na akenda mbali zaidi kuwa ugonjwa bado upo.

Angalau huyo aliongea hiyo juzi, ni baada ya hiyo taflani, kwa hiyo isingelitokea angelikaa kimya kama ambavyo Itilima, Bariadi wamekaa kimya, na waandishi wa Habari wamekaa kimya.

Serikali ione hili, itangaze kuwa ni janga katika mkoa wa Simiyu, viongozi wasikae kimya, Waziri wa Afya njoo Simiyu uone watu wanavyokufa, uone hali ilivyo, ugonjwa umekataa kutoka Simiyu, hii ni hatari, mtangaze, waandishi wa Habari tokeni mafichoni tangazeni hii hatari.

Watalaamu wa Afya wanajua kuwa hali ni mbaya, ila wanashindwa kusema kwa sababu viongozi wao wakuu wa serikali hawataki, ila watu wanaendelea kufa, kila siku lazima kifo kitokee na uzuri serikali imeweka kambi za wagonjwa hao katika kila Wilaya.

Kuendelea kuficha wakati watu wanaendelea kufa hii siyo sawa, Rais Samia watu wako wanakuficha, lakini ugonjwa umekataa kutoka Simiyu, itangazwe hali ya hatari Simiyu, kipindu pindu kimegoma kutoka, na hivi tunaelekea mwisho wa kiangazi, hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi.

=================


Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Faudhia Ngatumbura atoa neno vita dhidi ya ugonjwa wa kuhara na kutapika (kipindupindu) Wilayani Meatu.
Pia soma:
~
Wataalam wa Afya waingia mtaani kufanya jitihada za kudhibiti magonjwa ya kuhara Mkoani Simiyu
~ DC Meatu asitisha shughuli za Ibada Makanisa yasiyo na vyoo
 
Nipo huku. Ningetaja na vijiji ila naweza nikatekwa na kuuliwa pia humu mkaishia kusema bwana ametoa bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe
 
Issue ni Maji, Simiyu hakuna chanzo cha maji Safi na Salama ya kunywa kwa hio watu wanakunywa maji ambayo hayafai kwa afya ya binadamu hapo lazima uugue kipindupindu hata maji ya idara ya maji yanayopelekwa majumbani sio salama kwa kunywa,

Simiyu tatizo ni maji maji maji hata hayo maji yanayotoka idarani hayajafanyiwa treatment na watu wanapelekewa hivyo hivyo wengine wanakunywa bila kuchemsha wakihisi maji yametoka bombani basi ni safi na salama watoto, wanafunzi eeh wanakunywa maji ya bombani wakihisi maji yanayotoka bombani ni maji safi na salama kumbe maji yanakuja na tope

Kwa hio chanzo cha kipindupindu Simiyu ni ukosefu wa maji safi na Salama, Waziri wa Maji Juma Aweso sijui analijua hili au halijui hili?
 
Nipo huku. Ningetaja na vijiji ila naweza nikatekwa na kuuliwa pia humu mkaishia kusema bwana ametoa bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe
Watu wanakufa ila taarifa zinafichwa hii sio kabisa watu wanasema kwa kujifichaficha wanaogopa Serikali huu ujinga gani wakati watu wanakufa kweli
 
Tuwe makini sana na vyakula na maji haya maisha haya acha tu mengine kaa usimuliwe tu yasikukute yakikukuta nasikia tu yule nyumba ile kakata moto yaan turubai linatoka hapa linapelekwa pale hawajamaliza pale teyari mwingine kaanguka turubai linahamishwa halafu mamamae zenu mlivyo mamwehu na viongozi wenu wazembe wazembe hamsemi km ni kipindupindu kisa mnaleta siasa kwenye afya za watu hii nchi ya kisenge sana
 
Watu wanakufa ila taarifa zinafichwa hii sio kabisa watu wanasema kwa kujifichaficha wanaogopa Serikali huu ujinga gani wakati watu wanakufa kweli
Nilikuwa huko. Lakini watu.wala hawana habari kabisa minadani wanaendelea na maisha kama kawaida kula kula tu japo niliende kwa kuogopa ogopa
 
  • Thanks
Reactions: apk
Back
Top Bottom