zerominus10
JF-Expert Member
- Aug 25, 2022
- 8,142
- 13,721
Suala la kunya kunya sababu hawana vyoo hilo sikupingi mkuu huko kweli wanakunya Machakani hawachimbi vyoo sasa mainzi mainzi wanafanya transmission of diseases with no excuse, kwa hio Serikali iangalie hili wasiochimba choo aidha wachimbiwe au walazimishwe kuchimba vyooSimiyu hawajengi vyoo, wanakunya porini
Wabishi
Lakini wanataka huruma
Yaani uchimbiwe choo?? Hebu tuache ungeseSuala la kunya kunya sababu hawana vyoo hilo sikupingi mkuu huko kweli wanakunya Machakani hawachimbi vyoo sasa mainzi mainzi wanafanya transmission of diseases with no excuse, kwa hio Serikali iangalie hili wasiochimba choo aidha wachimbiwe au walazimishwe kuchimba vyoo
Kwani ile Kampeni ya Mrisho MPOTO na Banana Zoro ya kuhusu Nyumba ni Choo iliishia wapi Singida au Manyoni?Yaani uchimbiwe choo?? Hebu tuache ungese
Tunalea upuuzi…. Wanatia hasara kubwa serikali sababu ya uchafu
Nani kasema inasababisha kipindupindu? Kwanini umechagua kitu kimoja tu. Vipi nyama mbichi, maji machafu?Haisababishi kipindupindu
Muulize mmasai yoyote kuhusu ninayokwambia. Wewe ulikuwa unabisha Wamasai kunywa raw blood. It is their tradition. The thing is you don't know that is their culture, but you still want to argue childish stuffs. I was talking about Masai have certain immunity which you and I don't have and that is self evident. Childish , pointless conversation.Hahahaha ngoja nicheke ukimaliza nionyeshe makaburi yao
Ynahitaji serikali na ndiyo maana tunakuwa na serikali. Watu wote hawako sawa kwa upeo wa kuelewa mambo. Na pia kuna wajinga ambao wanaweza kudharau na kukataa kuzingatia kanuni. Hawa wote wanahitaji serikali iwaweke sawa kwa kutumia mifumo iliyopo.Chimbeni vyoo.
Usafi wa chakula na vyombo muhimu.
Watu wajenge vichanja vya kuoshea na kuanikia vyombo.
Haya hayahitaji serikali.
Kweli duniani kuna wapumbavu.Kuna vitu tukubaliane
1. Kipindupindu siyo Siri na serikali imepiga kambi simiyu kwahiyo kusema hawajali sio sawa….
2. Hakuna haja ya kupublicize aibu… kwani kipindupindu ni kula MAVİ, na mavi yanaliwa kupitia maji madharu… NINGEKUA KIONGOZI NINGEFUNGA KILA MWENYE KIPINDUPINDU
KabisaKweli duniani kuna wapumbavu.
Si wamepewa elimu na serikali wao au watoto wao ya kuwawezesha kutambua kanuni za usafi kuepusha magonjwa ya mlipuko? Wapuuzie wasubiri kushurutishwa wafe. Serikali haifi unakufa unaezembea.Ynahitaji serikali na ndiyo maana tunakuwa na serikali. Watu wote hawako sawa kwa upeo wa kuelewa mambo. Na pia kuna wajinga ambao wanaweza kudharau na kukataa kuzingatia kanuni. Hawa wote wanahitaji serikali iwaweke sawa kwa kutumia mifumo iliyopo.
Wapewe elimu, ila nalo litushinde? Sasa Mpox tutaiweze ikija?Nimekaa Bariadi watu wanakunya hovyo kama kuku. Sio ajabu kukuta kinyesi nje ya mgahawa. Wanyantuzu hawana kinyaa na kinyesi😔
Oya acheni utani wa kifala watu wanakufa Simiyu acheni utani wa kiduanzi iambieni Serikali yenu Simiyu kuna Kipindupindu wasilete utani
Mwaka huu pindua pindua Iko Nchi nzimaKwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu, nimesikia na kuona ugonjwa wa kipindupindu kushamiri wakati au majira haya ya kiangazi.
Hahahahahahahaha, kwanza inachekesha, lakini pia inahuzunisha, kwani watu wanakufa kweli kweli ingawa ni kimya kimya.
Iko hivi sasa, sikilizeni.
Mkoa wa Simiyu, ni moja ya mkoa ambao kipindi cha masika mwaka huu, wakati wa zile mvua nyingi, ulikumbukwa na ugonjwa au mlipuko wa kipindupindu.
Ugonjwa huu pia uliibuka katika mikoa ya Shinyanga, Mara, Mwanza, Kigoma, katavi, na mikoa mingi nchini, lkn baada ya zile mvua na kuanza msimu wa kiangazi ugonjwa ukatokomea.
Sasa cha ajabu na kushangaza, KIPINDU PINDU, Kimeisha kwenye mikoa mingine lakini Mkoani Simiyu, KIPINDU PINDU kimeganda na kuanza kumeshamiri vibaya sana.
Watu wanakufa, wengi wanapona, ni mamia ya watu ambao wamepata ugonjwa huu mpaka sasa, kwenye kiangazi kama hiki, kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinalipuka kama bomu, kimeua sana.
Kinachoshangaza zaidi, katika mkoa huo kuna Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya Habari, hakuna aliyetangaza, hakuna aliyeripoti ugonjwa huu wala chombo chochote cha habari ambacho kimeripoti ugonjwa huu.
Siyo waandishi tu, hakuna hata kiongozi yeyote wa serikali ambaye ametangaza uwepo wa hili janga ndani ya mkoa, wote wamekaa kimya na ugonjwa unaendelea kuua watu.
Kila siku watu wanakufa na huu ugonjwa, na taarifa zinasema ugonjwa umeshamiri Wilaya za Meatu, Itilima na Bariadi, na katika Wilaya ya Bariadi cha kuchekesha za ugonjwa umeshamiri na unaua Mjini, yaani Halmashauri ya Mji Bariadi.
Mpaka sasa mamia ya wananchi wa mkoa huu, wamekumbwa na ugonjwa huu kwenye hizo Wilaya na baadhi wamekufa, taarifa ambazo nazipata kila siku watu wanakufa kwa ugonjwa huu.
Juzi angalau nimena video ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu simjui jina, akieleza huo ugonjwa, na hiyo video ilikuja baada ya kutokea tafurani katika Wilaya hiyo, watu walilalamika kukamatwa na kutozwa faini kwa wale ambao walikutwa hawana vyoo.
Sasa kwenye hiyo taarifa Mkuu huyo wa Wilaya alisema baadhi ya watu wamekufa kwa ugonjwa huo, na wengine zaidi ya 60 wanaendelea kupatiwa matibabu na akenda mbali zaidi kuwa ugonjwa bado upo.
Angalau huyo aliongea hiyo juzi, ni baada ya hiyo taflani, kwa hiyo isingelitokea angelikaa kimya kama ambavyo Itilima, Bariadi wamekaa kimya, na waandishi wa Habari wamekaa kimya.
Serikali ione hili, itangaze kuwa ni janga katika mkoa wa Simiyu, viongozi wasikae kimya, Waziri wa Afya njoo Simiyu uone watu wanavyokufa, uone hali ilivyo, ugonjwa umekataa kutoka Simiyu, hii ni hatari, mtangaze, waandishi wa Habari tokeni mafichoni tangazeni hii hatari.
Watalaamu wa Afya wanajua kuwa hali ni mbaya, ila wanashindwa kusema kwa sababu viongozi wao wakuu wa serikali hawataki, ila watu wanaendelea kufa, kila siku lazima kifo kitokee na uzuri serikali imeweka kambi za wagonjwa hao katika kila Wilaya.
Kuendelea kuficha wakati watu wanaendelea kufa hii siyo sawa, Rais Samia watu wako wanakuficha, lakini ugonjwa umekataa kutoka Simiyu, itangazwe hali ya hatari Simiyu, kipindu pindu kimegoma kutoka, na hivi tunaelekea mwisho wa kiangazi, hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi.
=================
View attachment 3091759Pia soma:
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Faudhia Ngatumbura atoa neno vita dhidi ya ugonjwa wa kuhara na kutapika (kipindupindu) Wilayani Meatu.
~ Wataalam wa Afya waingia mtaani kufanya jitihada za kudhibiti magonjwa ya kuhara Mkoani Simiyu
~ DC Meatu asitisha shughuli za Ibada Makanisa yasiyo na vyoo
Naamini MillardAyo ataenda kufanya coverageOya acha utani kipindupindu kisikie hivyo hivyo kinapita na watu, pharmacy zimejazwa oral kimya kimya pumbavu hawawatangazii watu km kuna kipindupindu tho kuna redio nilisikia imejilipua wakatangaza kuna kipindupindu na watu wanakufa
Wasaidiwe tu watabidilikaSimiyu hawajengi vyoo, wanakunya porini
Wabishi
Lakini wanataka huruma
Utawasaidieje?Wasaidiwe tu watabidilika
Mbona rahisi sana mkuu, haraka harakaUtawasaidieje?
Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu, nimesikia na kuona ugonjwa wa kipindupindu kushamiri wakati au majira haya ya kiangazi.