Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Singapore kama moja ya nchi zilizo mstari wa mbele kwenye utunzaji wa mazingira duniani, imewahi kuwa na mikakati kadhaa ya kutunza usafi wa mazingira katika miji yake, huku kampeni ya mwanzo kabsa ikiwa ni mwaka 1958 ambapo walikuwa na kampeni kubwa ya KEEP YOUR CITY CLEAN, kampeni ambayo ililenga mahususi katika kuwaasa watu kuacha kutupa taka ovyo huku uongozi wa Halmashauri za Jiji zikisimamia mchakato mzima.
Mwaka 1959, serikali ilianzisha kampeni ya GERAKKAN PEMBERSEHAN BANDAR RAYA SINGAPURA ikiwa na maana Mchakato wa kusafisha Jiji la Singapore. Katika hotuba yake, Bwana Lee aliweka wazi kuwa nia na madhumuni ya kampeni hii ni kuwa msingi wa kwanza kabsa katika kulifanya Jiji la Singapore kuwa moja ya majiji yaliyo na usafi na unadhifu zaidi ndani ya bara la Asia.
Kuanzia mwaka 1960 imekuwa ni kawaida kwa Mamlaka za Jiji la Singapore kuendelea kupitia kampeni mbalimbali za usafi wa mazingira ndani ya Jiji hili, na lengo lako lilikuwa ni lile lile ambalo Bwana Lee alilionesha katika hotuba yake ya 23 Novemba mwaka 1959, na sasa wakaanza kuwekeza pia kwenye elimu ya kuwafanya watu wajua wajibu wao katika kutunza mazingira.
Agosti mwaka 1968 serikali kuu ilitangaza kuwa imeunda kamati ya kitaifa ya kampeni za mazingira, kamati ambayo itakwenda kufanya kazi ya kuifanya Singapore kuwa Jiji safi zaidi barani Asia na Duniani kwa ujumla, na kamati hiyo ilianza kazi yao mwezi Oktoba huku mwenyekiti akiwa ni Waziri wa Afya wa kipindi hicho, Mheshimiwa Chua Sian Chin, pia kamati ilikuwa na wawakilishi kutoka wizara kadhaa kama vile wizara ya Elimu, utamaduni, kazi pamoja na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi.
Je kamati ilianza kufanya kazi na kina nani?
1. Kwanza kabsa, kamati ilikaa chini ya vyombo vya habari, na kwa kuwa jambo hili lilikuwa ni la kitaifa basi vyombo hivi vilitumika kwa ukubwa wake kutangaza na kusambaza ujumbe huu. Kampeni ilikuwa ikisambazwa kwenye lugha nne, Kiingereza, Malay, Mandarin pamoja na Tamil, ambapo kulikuwa na mabango kwenye maduka yote, migahawa, ofisi za umma na binafsi, viwandani, vituo vya michezo, pamoja na mbao za matangazo.
Wizara zote zilishirikiana kuhakikisha mpaka tiketi za usafri zinakuwa na ujumbe kuhusu kampeni hii, stakabadhi za malipo, barua za kiserikali zilikuwa na ujumbe mmoja tu, KEEP SINGAPORE CLEAN.
2. Kupitia wizara ya Elimu basi kampeni ikapata kuingia masikioni mwa watu, kwani majukwaa ya elimu kwa umma yaliandaliwa kwa wingi, ambapo yalihusisha majadiliano pamoja na mihadhara kadhaa kutoka kwa viongozi mbalimbali. Pia elimu iliwafikia mpaka walioko majumbani kwani kulikuwa na kikosi kazi cha kuelimisha kuhusu kuweka jiji lao kuwa safi nyumba kwa nyumba.
3. Kupitia wizara ya mambo ya ndani, kampeni iliwapata elimu watu wote kuhusu faini na hatua za kisheria ambazo mtu atakutana nazo endapo akidharau agizo la serikali kuhusu kutunza usafi, huku wakiainisha kuwa faini ni dola 500, na ukikamatwa tena basi utalazimika kulipa faini ya 2000 , pia picha za mahala pachafu zilikuwa zikioneshwa ili kuwapa ile hisia ya sehemu chafu.
4. Kupitia wizara mbili za elimu pamoja na utamaduni waliweka mkazo na malengo mapana ya kuwaelimisha watoto wadogo kwani hili ndo kundi ambalo linakuwa na ndo taifa la kesho. Walipita mashuleni na kuwapatia madaftari pamoja na kuwafundisha kuhusu faida za kuwa na Singapore iliyo safi sana.
Baada ya kuonekana kuwa Jiji la Singapore limeanza kuwa na usafi wake ambao serikali ulitamani kuutazama basi wakaanzisha kampeni zingine ili kuboresha maeneo mengine ya kimazingira zaidi, mfano kampeni ya Tree Planting, Clean Water, huku pia wakianzisha kampeni za Please Keep My Park Clean pamoja na Keep Singapore Pollution Free.
Unaweza kujiuliza kwanini nimeanza na mapitio ya kampeni hizi kutoka Singapore?
Bila shaka tumekuwa mashahidi hapa nyumbani Tanzania, ambapo tumepata kushuhudia kampeni kadhaa za mazingira ambazo kiukweli zimeshindwa kuzaa matunda kabsa, kampeni ambazo hata wanaosimamia hawana uhakika kama zitaleta matokeo chanya, ni sawa na kubashiri kuwa kampeni itafanikiwa wakati tunaelewa malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira. Ni nani ambaye hajui kuwa Bahari ya India inachafuliwa kila sekunde na taka ambazo hutoka kwenye viunga vya jiji la Dar es salaam? Je ni nani ambaye hafahamu kuhusu ziwa Nyanza linavyochafuliwa na taka za kila aina kutoka mitaa ya Jiji la Mwanza?
1. Kuweka siku moja ya wiki ya usafi kitaifa.
Natambua na kushuruku kuwepo kwa siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa tufanye usafi kitaifa ila tokea Hayati Rais Magufuli amefariki ni kama siku hii imekosa tena nguvu na usimamiaji umekuwa hafifu sana. kwa fikra na mawazo yangu naomba tuwe na siku moja ambayo kuanzia saa 2 asubuhi tutafanya usafi kwa kina sio usafi wa mitandaoni au taarifa ya habari ya saa 2 usiku bali ni usafi kweli kweli. Katika usafi huo ndipo tutasafisha maeneo sugu ambayo yanapitisha taka hatarishi.

2. Kutenga eneo kubwa kwa ajili ya dampo na kuweka miundombinu ya kuchoma taka.
Serikali iweke sheria na kanuni ambazo zitafanya kila halmashauri kuwa na dampo ambalo litakuwa mbali na makazi ya raia, dampo hilo liwe na miundombinu yote rafiki ya kuhifadhi taka kuendana na uozaji wake. Kwa zile taka ambazo zinaoza ziweke mahala ambapo zitatumika kama mbolea huku zingine haswa zinazooza zikichomwa kwa teknolojia mpya kabsa ya Smokeless Pit iwe ni kutoka Solo Stove au Breeo, matanuru ambayo hutoa moshi kiasi kidogo sana.

3. Kununua magari mengi ya kuzoa taka
Ni suala la ajabu sana kuona tunanunua magari mengi ya Halmashauri, magari ambayo yanabakia kuwa yameegeshwa tu kwenye ofisi za Halmashauri siku nzima, wakati tunaweza kuwa na magari makubwa ya kukusanya taka kutoka madampo ya vijiji na mitaa na kuyapeleka kwenye dampo la mkoa. Mrudikano wa taka haswa zinazooza kwenye madampo ya mitaa na vijiji ndo huchafuka hali ya hewa kwa kiasi kikubwa.

4. Nne ni kuandaa kampeni za kitaifa kama walivyofanya uongozi wa Jiji la Singapore miaka ya 1960. Tuandae kamati ya kuhamasisha usafi wa mazingira huku tukizihusisha wizara zote katika hilo, sio tu NEMC na kumuachia mzigo wote Mhandisi Samuel Gwamaka.
Ninatamani sana siku moja mitaa ya Vwawa pale Songwe iwe safi kama vile makutano ya Mohammed V pale Tunis, ama mitaa ya Ilemela, Mwanza ikionekana nadhifu kama mitaa ya Guttenberg.

Natamani sana tupate kuwa na Tanzania safi.

Attachments
Upvote
2