Majibu ya Kiravu yanaonesha dhahiri kuwa kweli hatuna tume Tz. Hajui hata maana ya tume kuwa huru au kutokuwa huru! Mbona anajibu kama mtu asiyekwenda shule kabisa? Ushahidi wa kuibwa kura upo kihistoria, wagombea wameshawahi kulalamika mahakamani na wakashinda, na ushindi ukatenguliwa na mahakama (ubunge), kama wizi umeweza kufanyika katika ngazi ya ubunge ni dhahiri kuwa inaweza pia kufanyika kwa ngazi ya uraisi. Lakini pia watu wamekamatwa wakiwa na vifaa vya uchaguzi vikiwemo karatasi za kura, mihuri na hata mabox ya kura zilizokwisha kupigiwa mgombea mmojawapo, na hayo yakaripotiwa polisi. Anasemaje kura haziwezi kuibiwa? Hatuna tume Tz