Kisa cha Afisa mikopo na laana alopewa na mteja

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
8,797
Reaction score
25,177
Anachotaka Christine ni kupanda cheo hapa benki toka kuwa afisa mikopo mpaka kuwa meneja wa tawi.
Screenshot_20240416-211302.png

Anaamini akikaa hapo, wazazi matajiri wa 'boyfriend' wake watamheshimu na kumwona anafaa kuolewa na mtoto wao.

Lakini sasa shida ni moja, mfanyakazi mwenzake anayeitwa Stu.

Bwana huyu naye anakiwinda kiti cha umeneja kwa uchu mkubwa kwahiyo ni kama kuna vita ya chini kwa chini, kila mmoja akipambana kumvutia mkurugenzi ili alambe uteuzi.
Screenshot_20240416-211434.png

Mkurugenzi anamwambia Christine; "niskize bibie, una kila sifa ya kuwa meneja lakini kama kweli unakitaka cheo hichi, basi uwe mtu wa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya ofisi".

Christine anachukua 'desa' hilo na kulifanyia kazi. Alishataka vya uvunguni hivyo kuinama hana budi.

Unaambiwa engea engea na warina asali ili nawe upate kulamba vidole.

Majira ya mchana, anakuja mteja katika meza ya Christine, mwanamke mzee mwenye jicho moja bovu, jina lake Sylvia Ganush.
Screenshot_20240416-211533.png

Mwamamke huyu amekuja kuomba aongezewe muda zaidi wa mkopo wake kwani hana pesa ya kulipa kwa sasa, na nyumba yake aloweka dhamana bado anaihitaji.

Anaomba chonde chonde.

Maskini bibi huyu hajui amekuja muda mbaya sana, muda ambao Christine anapambania adhma yake ofisini.

Christine anamwambia haitawezekana maana muda alopewa ulitosha. Hata bibi anapiga magoti na kumsihi sana, nisaidie nisaidie. Anagoma kabisa!

Jibu ni muda unatosha, sina msaada zaidi.
Screenshot_20240416-211616.png

Inabidi 'security' waje kumbeba bibi na kumpeleka nje maana anaanza kuleta tafarani humu ndani. Amani inarejea na mkurugenzi anampongeza Christine kwa alichofanya.

Safi sana mwanetu, kaza hivyohivyo. Kiti cha umeneja kilee kinakuita.

Christine anafurahi asijue amejipalia makaa.

Baadae anatoka kazini kufuata gari lake parking. Kumbe bibi yule alikuwa akimngojea huko. Alipoingia kwenye gari, anashangaa anadakwa na mapambano makali yanazuka.

Christine anajaribu kujinusuru lakini si rahisi hata kidogo.

Hatimaye bi. Ganush anang'oa kifungo cha koti la Christine kisha anakinenea na kumpatia binti huyo kwenye kiganja cha mkono wake.
82fe6c6eba36b388984785b037c6fb52.png

Anamwambia: "Utanifuata ukiomba"

Christine anapoteza fahamu, kuja kuamka bibi hayupo.

Tangu hapo maisha yake yanabadilika moja kwa moja. Laiti angaliweza kumrudisha Christine wa zamani, hata kwa gharama yoyote ile, basi angalikuwa radhi.

Anahisi vitu vinavyomzunguka vimebadilika. Hayuko sawa. Anaongozana na mpenzi wake kwenda kwa 'mtaalam' ili wakatazame ustaarabu.

Aliyekwambia wazungu hawana haya mambo, nani?

Mtaalam anasema kuna kitu kikubwa kinamzengea Christine. Anairudisha pesa ya mteja, haitaki, na Christine anaondoka zake.
Screenshot_20240416-212036.png

Lakini sasa anaweza kulala?

Akilala, anakabwa.

Akikaa macho, anamwona bi. Ganush pembeni yake, nyuma yake ama mbele yake.
f7c69ad19d29220c0ae8a3a3de9cbe36.png

1d96c2c917636f3f2083ce5af1e4b029.png

Akitazama dirishani, anaona kivuli cha mnyama mwenye pembe kinakatiza. Mara kinasimama. Mara kinanyoosha mikono kutaka kumshika.
Screenshot_20240416-212336.png

Haijulikani upepo unatoka wapi. Mapazia hayatulii. Madirisha yanajifungua yenyewe!

Usiku unageuka kuwa 'series' ya kihindi, episodes mia saba na kumi.

Kesho yake kazini, anashangaa matone ya damu toka puani yanachuruzia kwenye documents za ofisi. Hajakaa sawa, anatapika damu kama bomba.
Screenshot_20240416-212429.png

Anapatwa na woga sana.

Anaona inatosha, anakimbilia nyumbani kwa bi. Ganush akaombe radhi, bibi nisamehe, haya ni makubwa sana kwangu.

Anapokelewa na mjukuu wa Ganush, lakini taarifa anayopewa si njema. Bibi alishakufa, hata hapo alipofika ndo' siku ya msiba wake.

Afanye nini?

Anarudi tena kwa mtaalamu.
Screenshot_20240416-212610.png

Screenshot_20240416-212445.png

Mtaalamu anatazama na kumwambia anazengewa na jini linaloitwa Lamia. Jini hilo hutumwa na mtu na huwa lina kawaida ya kumtesa mhanga wake kwa siku tatu kisha ya nne anaibuka na kumchukua mtu wake pamoja na kitu kilicholaaniwa vyote mpaka kuzimu!

Anamshauri ili kumpooza jini, inabidi atoe sadaka ya mnyama ili jini achukue nafsi ya kiumbe hicho na kumwacha yeye salama.

Christine anapofika nyumbani, anamtoa sadaka paka wake kipenzi. Anamchoma visu kisha anaenda kumfukia nyuma ya nyumba. Baada ya hapo, anapata amani. Anaona kazi imekwisha sasa.
Screenshot_20240416-212937.png

Anatoka na mpenzi wake kwenda ukweni kutambulishwa.

Kumbuka huku ukweni, hana 'CV' nzuri kwani anaonekana ni mtu wa familia ya chini hivyo anajitahidi sana kujenga wasifu wake hapa.

Haijapita muda, anaanza kuona maajabu katika meza ya chakula.
Screenshot_20240416-213115.png
Anavumilia ili asiharibu staha mbele ya wakwe zake lakini mara kidogo mambo yanashindwa kuvumilika.

Anapaliwa, kukohoa anatoka nzi!
Screenshot_20240416-213551.png

Mama mkwe anaachama kwa mshangao.

Mambo yanazidi kuparama na mwisho wa siku wanaondoka kwani kila kitu kinaharibika. Christine anaona maruweruwe.

Maruweruwe yasiyoonekana wala kuelezeka kwa wengine.

Anarudi kwa mtaalamu akiwa na hasira, mbona paka nimechinja kama manyaunyau? Mbona nimefata kama ulivyosema?

Ni nini sasa?

Mtaalamu anamwambia yeye amefika ukomo wake, na basi wakaonane na mwanamama San Dina. Yeye anaweza kumudu swala hili lakini inahitajika dola alfu moja.

Pesa si tatizo.

Wanaonana na mwanamke huyo akiwa na msaidizi wake na mbuzi mweupe. Mpango ni nini? Wamwite jini kisha waliingize kwenye mwili wa mbuzi na kumwangamiza.

Tambiko linafanyika na baada ya mapambano, jini linazama kwenye mwili wa mbuzi.

Panga linatupwa.

Nyiee! Nyiieee! Nyiee!

Panga linamkosa mbuzi, linakata kamba yake.
b4996e86f878f5c00fdf352e08ed24df.png

Mpaka jini kuondoka eneo hili, mtaalam San Dina yuko hoi bin taaban. Analazwa chini na si muda anakata kauli!

Christine anaambiwa bado jini halijatoka maana mbuzi wa kafara hakuchinjwa. Sasa suluhisho pekee ni kile kifungo kilicholaaniwa akamshikishe mtu mwingine mkononi.

Kwa kufanya hivyo ataihamishia laana huko.

Sasa ampe nani?

Baada ya kuwaza na kuchambua anaona mtu sahihi ni mfanyakazi mwenzake wanayeshindana, yaani bwana Stu lakini baadae anaingiwa na huruma.

Anaona mtu pekee wa kumpatia kifungo hicho ni bi. Ganush mwenyewe.

Anachukua chepeo na kwenda kaburini mwenyewe. Usiku mkali. Anaanza kufukua kaburi la mwanamke huyo udongo kwa udongo.

Atafanikiwa?

Tazama "Drag me to Hell".

55c552ad88a15f1f3bec7e77093f5cb5.png
 
Attachments

  • Screenshot_20240416-213441.png
    Screenshot_20240416-213441.png
    260 KB · Views: 18
Movies zote ninazozieleza hapa, kama umekwama, ingia Telegram search channel UZI MKALI, zipo zote humo.
 
Anachotaka Christine ni kupanda cheo hapa benki toka kuwa afisa mikopo mpaka kuwa meneja wa tawi.
View attachment 2965783
Anaamini akikaa hapo, wazazi matajiri wa 'boyfriend' wake watamheshimu na kumwona anafaa kuolewa na mtoto wao.

Lakini sasa shida ni moja, mfanyakazi mwenzake anayeitwa Stu.

Bwana huyu naye anakiwinda kiti cha umeneja kwa uchu mkubwa kwahiyo ni kama kuna vita ya chini kwa chini, kila mmoja akipambana kumvutia mkurugenzi ili alambe uteuzi.
View attachment 2965784
Mkurugenzi anamwambia Christine; "niskize bibie, una kila sifa ya kuwa meneja lakini kama kweli unakitaka cheo hichi, basi uwe mtu wa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya ofisi".

Christine anachukua 'desa' hilo na kulifanyia kazi. Alishataka vya uvunguni hivyo kuinama hana budi.

Unaambiwa engea engea na warina asali ili nawe upate kulamba vidole.

Majira ya mchana, anakuja mteja katika meza ya Christine, mwanamke mzee mwenye jicho moja bovu, jina lake Sylvia Ganush.
View attachment 2965785
Mwamamke huyu amekuja kuomba aongezewe muda zaidi wa mkopo wake kwani hana pesa ya kulipa kwa sasa, na nyumba yake aloweka dhamana bado anaihitaji.

Anaomba chonde chonde.

Maskini bibi huyu hajui amekuja muda mbaya sana, muda ambao Christine anapambania adhma yake ofisini.

Christine anamwambia haitawezekana maana muda alopewa ulitosha. Hata bibi anapiga magoti na kumsihi sana, nisaidie nisaidie. Anagoma kabisa!

Jibu ni muda unatosha, sina msaada zaidi.
View attachment 2965786
Inabidi 'security' waje kumbeba bibi na kumpeleka nje maana anaanza kuleta tafarani humu ndani. Amani inarejea na mkurugenzi anampongeza Christine kwa alichofanya.

Safi sana mwanetu, kaza hivyohivyo. Kiti cha umeneja kilee kinakuita.

Christine anafurahi asijue amejipalia makaa.

Baadae anatoka kazini kufuata gari lake parking. Kumbe bibi yule alikuwa akimngojea huko. Alipoingia kwenye gari, anashangaa anadakwa na mapambano makali yanazuka.

Christine anajaribu kujinusuru lakini si rahisi hata kidogo.

Hatimaye bi. Ganush anang'oa kifungo cha koti la Christine kisha anakinenea na kumpatia binti huyo kwenye kiganja cha mkono wake.
View attachment 2965787
Anamwambia: "Utanifuata ukiomba"

Christine anapoteza fahamu, kuja kuamka bibi hayupo.

Tangu hapo maisha yake yanabadilika moja kwa moja. Laiti angaliweza kumrudisha Christine wa zamani, hata kwa gharama yoyote ile, basi angalikuwa radhi.

Anahisi vitu vinavyomzunguka vimebadilika. Hayuko sawa. Anaongozana na mpenzi wake kwenda kwa 'mtaalam' ili wakatazame ustaarabu.

Aliyekwambia wazungu hawana haya mambo, nani?

Mtaalam anasema kuna kitu kikubwa kinamzengea Christine. Anairudisha pesa ya mteja, haitaki, na Christine anaondoka zake.
View attachment 2965788
Lakini sasa anaweza kulala?

Akilala, anakabwa.

Akikaa macho, anamwona bi. Ganush pembeni yake, nyuma yake ama mbele yake.
View attachment 2965790
View attachment 2965791
Akitazama dirishani, anaona kivuli cha mnyama mwenye pembe kinakatiza. Mara kinasimama. Mara kinanyoosha mikono kutaka kumshika.
View attachment 2965789
Haijulikani upepo unatoka wapi. Mapazia hayatulii. Madirisha yanajifungua yenyewe!

Usiku unageuka kuwa 'series' ya kihindi, episodes mia saba na kumi.

Kesho yake kazini, anashangaa matone ya damu toka puani yanachuruzia kwenye documents za ofisi. Hajakaa sawa, anatapika damu kama bomba.
View attachment 2965793
Anapatwa na woga sana.

Anaona inatosha, anakimbilia nyumbani kwa bi. Ganush akaombe radhi, bibi nisamehe, haya ni makubwa sana kwangu.

Anapokelewa na mjukuu wa Ganush, lakini taarifa anayopewa si njema. Bibi alishakufa, hata hapo alipofika ndo' siku ya msiba wake.

Afanye nini?

Anarudi tena kwa mtaalamu.
View attachment 2965792
View attachment 2965795
Mtaalamu anatazama na kumwambia anazengewa na jini linaloitwa Lamia. Jini hilo hutumwa na mtu na huwa lina kawaida ya kumtesa mhanga wake kwa siku tatu kisha ya nne anaibuka na kumchukua mtu wake pamoja na kitu kilicholaaniwa vyote mpaka kuzimu!

Anamshauri ili kumpooza jini, inabidi atoe sadaka ya mnyama ili jini achukue nafsi ya kiumbe hicho na kumwacha yeye salama.

Christine anapofika nyumbani, anamtoa sadaka paka wake kipenzi. Anamchoma visu kisha anaenda kumfukia nyuma ya nyumba. Baada ya hapo, anapata amani. Anaona kazi imekwisha sasa.
View attachment 2965796
Anatoka na mpenzi wake kwenda ukweni kutambulishwa.

Kumbuka huku ukweni, hana 'CV' nzuri kwani anaonekana ni mtu wa familia ya chini hivyo anajitahidi sana kujenga wasifu wake hapa.

Haijapita muda, anaanza kuona maajabu katika meza ya chakula.
View attachment 2965799 Anavumilia ili asiharibu staha mbele ya wakwe zake lakini mara kidogo mambo yanashindwa kuvumilika.

Anapaliwa, kukohoa anatoka nzi!
View attachment 2965798
Mama mkwe anaachama kwa mshangao.

Mambo yanazidi kuparama na mwisho wa siku wanaondoka kwani kila kitu kinaharibika. Christine anaona maruweruwe.

Maruweruwe yasiyoonekana wala kuelezeka kwa wengine.

Anarudi kwa mtaalamu akiwa na hasira, mbona paka nimechinja kama manyaunyau? Mbona nimefata kama ulivyosema?

Ni nini sasa?

Mtaalamu anamwambia yeye amefika ukomo wake, na basi wakaonane na mwanamama San Dina. Yeye anaweza kumudu swala hili lakini inahitajika dola alfu moja.

Pesa si tatizo.

Wanaonana na mwanamke huyo akiwa na msaidizi wake na mbuzi mweupe. Mpango ni nini? Wamwite jini kisha waliingize kwenye mwili wa mbuzi na kumwangamiza.

Tambiko linafanyika na baada ya mapambano, jini linazama kwenye mwili wa mbuzi.

Panga linatupwa.

Nyiee! Nyiieee! Nyiee!

Panga linamkosa mbuzi, linakata kamba yake.
View attachment 2965802
Mpaka jini kuondoka eneo hili, mtaalam San Dina yuko hoi bin taaban. Analazwa chini na si muda anakata kauli!

Christine anaambiwa bado jini halijatoka maana mbuzi wa kafara hakuchinjwa. Sasa suluhisho pekee ni kile kifungo kilicholaaniwa akamshikishe mtu mwingine mkononi.

Kwa kufanya hivyo ataihamishia laana huko.

Sasa ampe nani?

Baada ya kuwaza na kuchambua anaona mtu sahihi ni mfanyakazi mwenzake wanayeshindana, yaani bwana Stu lakini baadae anaingiwa na huruma.

Anaona mtu pekee wa kumpatia kifungo hicho ni bi. Ganush mwenyewe.

Anachukua chepeo na kwenda kaburini mwenyewe. Usiku mkali. Anaanza kufukua kaburi la mwanamke huyo udongo kwa udongo.

Atafanikiwa?

Tazama "Drag me to Hell".

View attachment 2965803
Mmh hii unaangalia huku unajifunika macho,inaonekana tamu kwel
 
Back
Top Bottom