Ajali ya mwendokasi ilyotokea wiki moja iliyopita maeneo ya Kisutu ina shangaza mengi!
Ajali ile ilitokea majira ya asubuhi na kuhusisha gari dogo kugongana na mwendokasi ulikochangia majeruhi kadhaa akiwemo bwana mmoja aliyekuwa mtembea kwa miguu (Osman)
Taarifa za vyombo vya habari, report za hospital na report za kipolisi zilieleza wazi kila kitu kilichojiri (sitarudia)
Takribani karibu siku saba baadae zimepita hadi Jana 27 February 2023! Taarifa za hospital ziliendelea kueleza HAKUNA MTU aliyejitokeza kwenda kumtambua mhanga wa ajali (bwana OSMAN)
Baada ya taarifa ya hospital kutaja kwamba yule mtu kazinduka! Ufahamu umerejea! Leo tarehe 28 ndipo Tunamshuhudia mke wa Osman pamoja na ndugu akijitokeza kumtambua (Yote ni kheri ya Mungu).
Tunashukuru ndugu wamepatikana, lakini kupatikana kwao kwa vyovyote vile kunaibua maswali mengine ingawa tunashukuru wamepatikana!
Simulizi za mke wa Osman!
Mama huyu kwa mara kwanza kasikika akisimulia kwamba hakuwa na taarifa Yoyote hadi pale shemeji yake jana alipomtaarifu kwamba, Taarifa za hospital zinazomtaja OSMAN (wanahisi Osman anayetajwa kupata nafuu hospital ni ndugu yao)!
Mke wa OSMAN Anaendelea kusimulia kwamba, Siku ya tukio, mmewe alimuaga kama kawaida yake kwamba anakwenda kibaruani (kwamba OSMAN anajishughulisha na kubeba mizigo hapo Ferry) kwamba alimuaga kuwa huenda anatarajia kusafiri na chombo siku hiyo kwa siku kadhaa!
Haya ni maelezo ya mkewe OSMANI!
Maelezo hayo yana ukweli mwingi kwamba huenda ni kweli kwamba alijua mme wake kasafiri ndiyo maana hakuwa na wasiwasi kwamba atarudi!
Lakini maelezo hayo hayawezi kuwa kweli pasipo kusindikizwa na style yao ya maisha, history, uhusiano wao kama familia!
Ni kweli alisafiri kama alivyoaga, je baada ya siku ya kwanza, ya pili ya tatu mke na ukoo wao wote na majirani hawakuona ya mtandaoni kiasi cha kushtuka?
Sawa mke hana simu, je majirani na ndugu hawakuona angalau kufananisha fananisha?
Majibu ya hayo yote ni mepesi tu kwamba UMASKINI HULETA TABIA YA KINYAMA! Ninaposema tabia ya kinyama sina maana tabia ya kikatili bali namaanisha Umasikini huzalisha tabia ya kutojali!
Tunashukuru ndugu wamepatikana lakini YAMKINI ...na may be ....Havitaacha kugonga vichwani mwa watu wengi.
Yote kwa yote mipango ya Mungu haina makosa, Na kila uzao hauwezi kupatikana pasipo kutungwa mimba!
Ajali ya mwendokasi ilikuwa mimba ya kumuumba OSMAN MPYA!
Mimba ile ilutungwa kwa mwenye gari dogo! Taarifa za kipelelezi zinaonesha yule mwenye gari dogo alikuwa na mgogoro na mkewe uliomjaza stress!
Stress za mapenzi kwa dreva wa gari dogo zilimfanya apoteze umakini barabarani (uzembe)
Hadi pale alipokatiza hovyo na kugonjwa na mwendokasi! Kulikopelekea gari la mwendokasi kwenda kumgonga bwana OSMAN!
MBIO ZA YULE MLINZI HAZIKUWA NA FAIDA, BALI MIMBA Ile ilikuwa kwa ajili ya kumzaa OSMAN MPYA!
Tumuombee apone mapema!
USHAURI!
1. HOSPITALI ZINAPOTANGAZA KUTAFTA NDUGU wasiache kutamka wazi kwamba HAKUNA DENI WALA BILI KWA NDUGU! Ikiwezekana anayejitokeza waseme watamsaidia kumsafirishia mgonjwa hadi nyumbani! (Hili litasaidia watu wasiwe wanauchuna na kutelekeza ndugu na jamaa)
2. NIDA waboreshe taarifa za vidole na database! Kwamba alama za vidole ziwekwe kwenye kanzidata ya taifa ili hospitali wakiskani vidole taarifa za mtu na ndugu zijazwe huko.
Heri maskini wa roho kuliko maskini wa mali maana ni rahisi sana kukosa ufalme duniani na mbiguni!
Tubuni na kuiamini injili

- YAMKINI KWASABABU YA UMASKINI huenda ndugu na jamaa waliamini yule jamaa kakata moto hivyo wakaamua kukausha! (May be)
- YAMKINI kwakuogopa bili ya hospitali (gharama za matibabu) mke, ndugu na jamaa waliamua kukausha! (May be)
- YAMKINI kwa tabia za maisha yao ni kama UMEME WETU, kwamba mme akiondoka haagi na akirudi tunashangilia huooo! (May be)
- YAMKINI SASA BAADA YA KUSIKIA KAZINDUKA (OSMAN) Familia na ndugu wameogopa kwamba atawaumbua kwa kuwataja! Hivyo sasa wamejitokeza chapu! (May be)
- YAMKINI huyu wameona huyu mtu kapona sasa huenda kuna matunda mbele ya misaada (may be)