Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Asha alizaliwa katika kijiji kilicho kando ya bahari. Shughuli kuu katika kijiji kile ilikuwa uvuvi na Kilimo.
Asha alipenda sana kula samaki lakini aliona aibu kulisema hilo na badala yake alisema hapendi kula samaki.
Wazazi wake walihangaika kutafuta mboga mbadala kwaajili ya mtoto wao kila walipopika samaki.
Siku moja watu wote wakiwa shambani Asha alirudi nyumbani kwa siri ili akale samaki aliyebaki kwenye maakuli ya jana yake. Kwa hamu kubwa aliyokuwa nayo Asha alikula samaki kwa pupa na hii ilipelekea kukabwa na mwiba wa samaki.
Asha alikuwa kwenye maumivu makali wazazi wake waliporejea na ilibidi apelekwe hospitali.
Wazazi walibaki na mshangao tabibu alipotoa mwiba wa samaki kwenye koo la Asha.
Njia ya mwongo ni fupi.