Kisa cha Asha na msiba wa samaki

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Asha alizaliwa katika kijiji kilicho kando ya bahari. Shughuli kuu katika kijiji kile ilikuwa uvuvi na Kilimo.
Asha alipenda sana kula samaki lakini aliona aibu kulisema hilo na badala yake alisema hapendi kula samaki.
Wazazi wake walihangaika kutafuta mboga mbadala kwaajili ya mtoto wao kila walipopika samaki.
Siku moja watu wote wakiwa shambani Asha alirudi nyumbani kwa siri ili akale samaki aliyebaki kwenye maakuli ya jana yake. Kwa hamu kubwa aliyokuwa nayo Asha alikula samaki kwa pupa na hii ilipelekea kukabwa na mwiba wa samaki.
Asha alikuwa kwenye maumivu makali wazazi wake waliporejea na ilibidi apelekwe hospitali.
Wazazi walibaki na mshangao tabibu alipotoa mwiba wa samaki kwenye koo la Asha.

Njia ya mwongo ni fupi.
 
Hii tabia na uzee wangu ninayo. Hasa linapotokea suala la mwanamke mzuri mrembo anayenibamba roho kisawasawa.

Kwenye kadamnasi humponda na kumshusha sana, wakati nikijitahidi kumfuatilia hadi nimpate.

Ukweli wa upendo wangu na ninavyomshobokea huuungama nikiwa naye faragha nimeshampata.
 
Hadith Inanikumbusha Vutabu Nnavyovipenda Vya Alf Laylah Wa Laylah,"One thousand And One Days"
Ndo Kwanza Niko Volume ya 1 Bad Nyingine 5. Hakika Kisa Hiki Kinaendana Kabisa Na Visa Vya Kina Khalifa Haroun Al Raschid

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Dah....kila nikiupitia huu uzi naelewa tofauti....umeandikwa kwa kificho sana.....nimeupitia mara 20....ngoja niuache sasa...maana naelekea kuitwa mchochezi 🙂🙂🙂
 
naomba ntumie soft copy
 
Ndg yang umenkumbusha mbali Sana nilikua na rundo la vitabu hivo nkamuazima jamaa ckumuona tena.Roho yauma naeza pata wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…