Kisa cha Harmonize kukimbia WCB Wasafi na kisa cha Dogo janja kumkimbia Madee Ali

Kisa cha Harmonize kukimbia WCB Wasafi na kisa cha Dogo janja kumkimbia Madee Ali

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
183
By Sangu J

Kama nilivyokiri awali kwenye Makala yangu kwamba mimi ni mshabiki mkubwa wa @wcb_wasafi na wasanii wote waliokuwepo humo, na kueleza mambo ambayo Harmonize ili aweze kufanya vizuri nadhani yalikuwa na umuhimu ya kufanya, ili aweze kupiga hatua kwa sasa kama ulikosa unaweza kurudi kwenye post zangu za nyuma, na kujisomea.
.
Leo kisa cha Harmonize kukimbia @wcb_wasafi iwe kwa wema au ubaya, lakini imenikumbusha kipindi ambacho @dogojanjatz ambaye aliamua kutoka chini ya mikono ya @madeeali na kuamua kwenda kujitafutia maisha yeye mwenyewe, na akakumbatiwa na mikono ya Ustadhi Juma na Musoma.
.
Nakumbuka kipindi hicho hakuna ambaye alikuwa hajui wapi ambapo Madee alikuwa amemtoa Dodo Janja, ambayo kimtazamo fulani inafanana na namna ambavyo @diamondplatnumz alimpata Harmonize na kuamini aingie ndani ya WCB.
.
Njia ambayo Dogo Janja, kwa wakati huo aliondoka kiuhalisia haikuwa nzuri ndiyo maana, hata alitoa wimbo wa Yamoyoni na kueleza mambo ambayo alikuwa akifanyiwa chini ya Madee, na kwenye nyimbo kundi ya Watasubiri bado Janjaro alitamba kwamba aliondoka chini ya Madee na alienda kwa Ostadhi Juma, kw ausafiri wa ndege.
.
Sasa turudi kwa Harmonize kwanza njia aliyoondoka nayo iliaminika kwamba ilikuwa ya amani sana pale WCB lakini kwa mazingira ya sasa inaonekana hali si shwari kabisa, kuna mahali kuna tatizo,
.
Mimi sina mashaka na kipaji cha Harmonize asilimia 100, ila tatizo ni aina ya Uongozi wake mpya aliokuwa nao, utamfanya afikie kule ambapo tulitegemea afikie, hata Janjaro alikuwa na kipaji kikubwa sana, ila tatizo ni menejiment aliyokuwa baada ya kutoka Madee ilishindwa kumfanya awe mkubwa hasa baada ya kushiriki ngoma mbili tu.
.
Sasa najiuliza kama kilichomkwamisha kipindi Kile Janjaro kilikuwa ni uongozi, sasa najiuliza je uongozi mpya wa Harmonize una uzoefu na kujua code za muziki wa Bongo, na je uzoefu huo ameupatia wapi, kwa wasanii gani, amba aliwahi kuwasimamiana walifanya vizuri sana Bongo.
.
Wote tunajua historia ya Mkubwa Fella na Babu Tale kwenye kusimamia wasanii na wengi wao mpaka sasa bado wanafanya vizuri, sasa je huyu wa Harmonize anaweza kweli, kumsaidia Harmonize kumpigisha hatua zaidi ya aliyofika akiwa chini ya WCB.
.
Muziki wa Bongo hauhitaji pesa ili upenye masikia ya watu inahitaji kujua mbinu tu, kwa sababu hata Otashi Juma alikuwa na pesa lakini alikosa mbinu za kumkuza Dogo Janja na baadaye alirudi kuomba msamaha, kwa Madee na alisemehewa.
.
Simuombei Harmonize kufeli lakini nadhani pia, hichi kisa cha Harmonize na Diamond Platnumz, kimenikumbusha kisa cha Dogo Janja na Madee.
.
#KijanaMzalendo
#WCBForLife
#MaoniYangu
 
Siku Hamonize akitoa wimbo kila kitu kitabaki uchi kwa sasa tutaongea mengi lakini wakati utasema kweli.
Combination ya Fella+Tale+Sallam ni future ya entertainment industry ningekuwa ni mimi nisingekaa mbali na awa watu.
 
Umenikumbusha ya Rostam na timu ya wananchi (mpira na rost wapi na wapi) dhidi ya chuki kwa Mo
 
[emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211]eeh afu ndie msanii pekee hits zake kali zote ni alizo shirikiana na platnumz.. na aka ishia kufunikwa...vipi ukitoa izo kuna nyingine iliyo fikia mafanikio zaid ya izo za #bado na #kwangwaru
Lazima Wamuwaze Maana,

Alikuwa Anaongoza Kwa Kuingiza Mapato WCB,

Ndio Msanii Mwenye Nyota Kali WCB Kwa Kutoa Hits Ambazo Diamond Mwenyewe Akawa Analazimisha Awemo Kama Kolabo Ili Aendelee Kusikika
 
Siku Hamonize akitoa wimbo kila kitu kitabaki uchi kwa sasa tutaongea mengi lakini wakati utasema kweli.
Combination ya Fella+Tale+Sallam ni future ya entertainment industry ningekuwa ni mimi nisingekaa mbali na awa watu.
Salaam Anamsimamia AY Hatuoni Jipya !
Kwa Navy Kenzo Hatuoni Jipya !
Babu Tale Ni Takataka, Anasafiria Nyota Ya Abdu Bonge.
Wasanii Waliopita Kwake Kibao Na Hawana Jipya Lolote.
Kila Mtu Kwenye Maisha Ana Nafash, ACHENI KUABUDU WATU !
 
Lazima Wamuwaze Maana,

Alikuwa Anaongoza Kwa Kuingiza Mapato WCB,

Ndio Msanii Mwenye Nyota Kali WCB Kwa Kutoa Hits Ambazo Diamond Mwenyewe Akawa Analazimisha Awemo Kama Kolabo Ili Aendelee Kusikika
Mhhhhhh.
 
Usichokijua ni

Dogo janja wakati yupo chini ya madee, karibia nyimbo zoote alitungiwa na madee ikiwa pamoja na na promo na kila kitu na ndomana wakati ule mistari ya wakati ule ilikua ya kiutu uzima ilikua tofauti na umri wake

Ukija kwa hamo , hamo amemsaidia sana diamond hasa kwenye uandishi, hata style za melody hamo amempita dai mbali sana

Mziki wa dai ni mwepesi sana na ndio maana bila kick za insta aufiki mbali
 
Manager wake ni mwanamke mmoja anajiita mjerumani, tangu yupo wasafi, utofauti utakuwa upi?
 
Diamond alimchukua harmonize kwasababu alimuona ni threat kama atakua atakuja kumfunika. Ila harmonize ajiangalie sana jembe ni jembe ni mnafiki sana atakuja kumuacha kwenye mataa atashangaa. WCB wanaweza kumkuza mbosso kuja kuziba pengo la harmonize
 
Back
Top Bottom