Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Katikati ya mbuga ya wanyama ya Arbedare iliyopo nchini Kenya, kuna hoteli inayoitwa Treetops. (Pichani).
Humo ndimo Eliza alitwaa kiti cha Umalkia wa Uingereza na kupata hadhi ya kuitwa Malkia Elizabeth II mnamo mwaka 1952 punde tu baada ya kupokea taarifa za kifo cha baba yake, King George VI.
Kwa desturi za utawala wa Uingereza, kiti cha mfalme/malkia hakipaswi kuwa na wala hakijawahi kuwa wazi. Ndio maana, kufuatia kifo cha malkia hapo juzi, bendera zote za uingereza ikiwemo bendera ya taifa, zilipepea nusu mlingoti ISIPOKUWA bendera ya kifalme "Royal Standard", ambayo huwa haipepei nusu mlingoti kuashiria kwamba "utawala wa kifalme bado unaishi" kwani aliyekufa ni mtu na sio utawala.
Hivyo, mwaka Elizabeth II alitangazwa 'proclaimed' kuwa malkia wa Uingereza akiwa nchini Kenya kwenye hotel ya Treetops.
Alikuja kutawazwa 'coronated' mwaka mmoja baadae, 1953, huko Uingereza katika jumba (kanisa) la Westminster Abbey.
Baada ya kutawazwa, Malkia aliagiza kwamba kapeti (zulia) lililotumika katika sherehe za kutawazwa kwake, likatwe na kipande kipelekwe nchini Kenya kwenye kanisa la Mt. Philip, ambapo alifanya ibada siku moja kabla ya kifo cha baba yake. Kapeti hilo lenye rangi ya bluu, lipo hadi leo limehifadhiwa hapo.
Wakatabahu
©KichwaKikuu