Kisa cha kweli: Jinsi nilivyosengenywa na "kubaguliwa" na Watanzania wenzangu nchi ya ugenini

😀😀😀😀mheiwe.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mwisho mkaanza kunusana nyie wenyewe haaa haa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii umenikumbusha mbali saaana.

Mimi haikuwa kwa mweusi mwenzangu bali ilikuwa ni kwa wazungu. Tulikuwa ufukweni tunapunga upepo na tulikuwa watanzania watatu na wakenya wawili. Kati yetu wanamme tulikuwa watatu na wanawake wawili. Lakini hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi kati yetu wote.

Walikuja mwanamme na mwanamke na watoto wawili nao wakakaa jirani na sisi. Tuligundua kuwa huyo mke na mme ni mtu na mmewe kutokana na maongezi. Kiss kwa wingi. Lakini mme alikuwa ni kijana mdogo nae mke umri ilikuwa umeende.

Kama kawaida wamama tuliyokuwa nao wakaanza kuwakogoa wanandoa hao kuwa mme kamuoa dada yake. Wanamme ikawa tunasema kuwa ni kawaida kwa wazungu lkn kina mama waliendelea kuwasemea mbovu za kutosha. Kilichowaudhi ni pale mwanamama wa kizungu aliposimama mimi nikasema "kweli huyu mama kazeeka hadi matako yake yamepolomoka"

Kauli hiyo iliwaudhi kumbe wanaelewa kiswahili vizuri sana wote mke na mme. Walitutolea mbovu tukawa kimya kama tumemwagiwa maji ya baridi. Huku wakisema "tena wote hawa ni watanzania wenzetu"

Tuliwaomba msamaha na kwa kweli walitusamehe kumbe wote wamezaliwa na kukulia palokia moja huko makete iringa. Tulijiona choo sana nchi ya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu unamoyo wa kipekee ingekuwa mimi nisungewaacha salama


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…