Kisa cha Marehemu Sauli na Dereva wa lori kilichotokea mwaka 2020

Kisa cha Marehemu Sauli na Dereva wa lori kilichotokea mwaka 2020

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Ukitaja kufanikiwa kibiashara jitofautishe na wenzako kwa kufanya tofauti lakini bora

Mabasi ya Sauli yalijitifautisha kwa kutopoteza muda kizembe barabarani ....TIME MANAGEMENT !!!

Solomon Sauli hatunaye amefariki ajalini na ameshazikwa kijijini kwao.

Mwamba hakufa kizembe,wake watatu na watoto 16.

Mwaka 2020 Sauli akitokea Mbeya akiekekea Dar es salaam,maeneo ya check point ya Ruaha Mbuyuni karibu na daraja la mto Ruaha linalotengabisha wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa na Kilosa mkoa wa Morogoro,.

Mbele yake linapita lori tupu wanaita tenga,likiwa halina mzigo wowote,

Kutoka Ruaha kuna kijiji kinaitwa Kidai kabla ya kufika kona za Iyovi,huwezi kuamini ndugu msomaji lile lori lilikuwa linakimbia sambamba ba gari ndogo alilokuwa akiendesha bwana Sauli,kona za Iyovi huwa sio za kitoto ni hatari sana lakini dereva wa lori akikuwa analala nazo kana yuko tambarare.

Wakiwa wanakaribia mikumi marehemu Sauli alikanyaga mafuta hasa na kulisubiri lori pale mzani,
Walichoongea hakuna ajuaye ila baada ya wiki moja yule dereva wa lori alikabidhiwa basi la Sauli,

Tuliotumia hiyo njia tulikuwa tukipanda hilo basi lazima utubu dhambi zako ukiwa safarini
 
Back
Top Bottom