Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Malaika aitwaye Makerubi alikuwa na kazi ya kumsifu Mungu Mbinguni, sifa kubwa ya malaika hawa huwa na mbawa sita ambazo mbili zina uwezo wa kumfunika mwili mzima.
Kwa nini Mungu aliwaumba? Mungu aliwaumba kwa sababu alitaka kusifiwa milele. Mungu anapenda kuabudiwa na humbariki mtu anayefanya hivyo. Lengo kubwa la Mungu kutuumba ni kumsifu na kumuabudu. Hakuna kingine.
Ukisoma kwenye Biblia imeandikwa kwamba hata sisi tusipomsifu, atayainua mawe yamsifu, hakuna tatizo kwenye hilo.
Kwa sababu malaika hawa walikuwa wakimsifu Mungu, kuna siku malaika mmoja kiongozi wa Makerubi akaona kama zile sifa alitakiwa kuzipata yeye na hivyo kuwaita wenzake na kupanga mchongo wa kumpindua Mungu. Alitaka kukalia yeye kiti cha enzi.
Baadhi ya malaika wakakubaliana naye lakini akahisi kama angesalitiwa, hivyo kuwaamuru waape, wakaapa kwamba hawatomgeuka.
Mungu hapigani vita yeye, ana malaika zake ambao ndiyo hupigana vita wakiongozwa na malaika mwenye nguvu aitwaye Mikaeli. Huyu malaika ameonekana sehemu nyingi vitani, aliongoza vita ya kuuchukua mwili wa Musa jangwani na kuuzika, aliongoza vita dhidi ya Leviathan. Hii nilizungumzia huko nyuma, walikuwa wawili, Mungu akataka kuwamaliza kwa kuwa walionekana kuwa tishio kwa dunia huko mbeleni.
So huyu Mikaeli ni malaika wa vita ambaye muda wowote yupo tayari kupokea amri ya Mungu ni wapi aende kukiwasha.
So baada ya malaika kupanga michongo yao, Mikaeli na malaika wengine wakapambana na hao makerubi na kuwashinda, hivyo wakatupwa kuzimu, yaani hawakustahili hata kukaa dunia, Mungu akatengeneza sehemu iitwayo Sheol na kuwatupa huko. Wamezungukwa na maji.
Sasa baada ya kukaa huko, wakawa wanapata muda wa kutembea duniani. Hawa malaika waliotupwa huko, miili yao ikabadilika na kuwa majitu ya kutisha, na ndiyo maana hakuna jini mwenye sura nzuri.
Walipokuwa wakija duniani, wakawa wanatransform miili yao na kuwa na miili ya binadamu na hatimaye wakawatamani wanawake duniani na kufanya nao mapenzi, hatimaye wakafanya nao mapenzi na kuzaa mijitu mikubwa.
Hebu subiri kwanza!
Haya mashetani yalitoka mbinguni, yaani yalikuwa yakikaa karibu na Mungu. Kwa maana hiyo walikuwa wakijua siri zote kuhusu Mungu, walijua ukitaka kupambana na Mungu, ufanye nini, wanajua ukitaka kumkera Mungu ufanye nini.
Unaposikia shetani, si kitu kidogo, ni likiumbe likubwa na lenye nguvu. Kivipi?
Wakati Yesu alipokuwa duniani, kila alipokuwa akimkaribia mtu mwenye mashetani (mapepo) alikuwa analia kwa maumivu, mapepo yalikuwa yakiumia, lakini huyu shetani, alikuwa na nguvu mpaka za kuzungumza na Yesu na kumjaribu.
Yaani alikuwa karibu naye, walizungumza na kumjaribu, Yesu akawa anamjibu kwa vifungu vya vitabu. So hapa jua kwanza nguvu ya hili lijamaa lilitotupwa kutoka kuzimu.
Okay!
Tuendelee.
Hapa natumia neno mashetani kwa kuwa tayari yalipelekwa kuzimu. Yalipokuja, yalikuwa na siri kubwa za Mungu, wakataka kuwagawia binadamu, yaani nao wawe na kauwezi hata kidogo kama alichokuwanacho Mungu.
Wakaleta uchawi. Yaani ule uweza wa Mungu, nao walikuwa wakiuchukua kama ule halafu walifanya mambo makubwa hapa duniani. Sasa hapo ndipo Mnara wa Babel ulipoanza kujengwa.
Nimeruka sana mpaka kuja Babel, ila endelea kunifuatuilia.
Kwa hiyo watu wakafundishwa kutengeneza silaha, wakafundishwa uchawi, wakafundishwa kuhusu masuala ya anga (akina NASA hawa), walifundishwa kila kitu, na wakaanzisha dini zao.
Sasa hapo Babel kukawa na mfalme mmoja mwenye nguvu kubwa, huyu aliitwa Nimrod. Nimrodi alikuwa na nguvu kupita kawaida.
By then, mataifa yote duniani yalikuwa yakilipa ushuru wake hapo Babel. Hii Babel sasa hivi ipo Kusini mwa Mto Mesopotamia, mji wa Hillah huko Babil, Iraq.
Kwa hiyo huyu Nimrodi alikuwa ni kizazi cha hao majitu makubwa, akataka kupigana vita na Mungu, alitaka kumpiga Mungu.
Hapo ndipo akaamua kujenga mnara wa Babel.
Hebu subiri.
Hapa ndipo tunapochanganya vitu. Jamani! Mnara uliojengwa hapa haukuwa mnara kama unavyoujua. Yaani halikuwa jengo kama la Burj Khalifa
Hapa ndipo tunapokuja na kujuzana kwamba Biblia haitakiwi kusomwa kama gazeti, kuna mambo mengi ndani yake imeandika, ili upate muongozo, utatakiwa kusoma vitabu vingine kwa undani.
Mnara ukajengwa, ila haukuwa mkubwa, ulikuwa mpana sana kama nyumba kwa juu, na kule ndipo walipokuwa wameweka mavitu yao ya uchawi ambayo waliambiwa yangetumika kupambana na Mungu.
Kumbuka kipindi hicho Babel ilikuwa ikifanya mambo makubwa, ilifufua mpaka watu, iliponya watu magonjwa, yaani ilikuwa ni chimbuko la kila kitu, mpka serikali, na hizi dini za kumuabudu shetani.
So kule juu kulikuwa na matambiko yao, walikuwa wakipambana na Mungu, walitaka kumuona Mungu. Bulj Khalifa ni mnara mkubwa sana , mara tatu ya Babel ila ilizungumziwa urefu wa kutaka kumfikia Mungu kwa matambiko.
Watu walipambana, uchawi ulioletwa na wale malaika ukatumika kutaka kupigana na Mungu, wakataka kufika mpaka mbingu ya saba. Na vitabu vilieleza kwamba uchawi wao ulifanyika kwa nguvu mpaka mbingu ya pili hivi lakini Mungu alivyokuwa fundi, akawachanganyia lugha.
Chimbuko la lugha likaanzia hapo. Sasa matambiko yalikufa kwa kuwa watu hawakuwa wakielewana, unaambiwa lete tunguli, wewe unampa mtu upanga.
Sasa watu wakatawanyika, wakatafutana wale waliokuwa wanaelewa lugha fulani, wakaenda kuunga nchi zao. Yale matambiko yakaishia hapo japokuwa baadaye Babel iliendelea sana mpaka Alexander The Great kwenda huko na kufia mjini humo.
Kutokana na uimara wa huyu jamaa, kifo chake kimetangazwa kwa njia mbili. Biblia na vitabu vingine vinasema Esau (Mjukuu wa Abraham) ndiye aliyemuua Nimrodi kwa kumchinja lakini Kurani inasema jamaa alikufa baada ya kuingiwa na mbu sikioni na kupita mpaka kwenye ubongo wake na kuanza kujipigiza kichwa mpaka kifo chake.