Ni kisa cha kusikitisha ambacho kimemkumba Peter Oloo Aringo Junior mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa maarufu Kenya Mzee Peter Oloo Aringo aliyepata kuhudumu kama mbunge na waziri ktk serikali ya Kenya.
Kama tujuavyo wanasiasa wa Kenya waliofikia ngazi za kuhudumu ktk baraza la mawaziri wengi wao huishi maisha ya ufahari mkubwa usioweza kufikirika kutokana na kuweza kuendesha biashara kubwa kupitia mgongo wa afisi za umma.
Lakini kama wazee wasemavyo kua uyaone, kisa cha mtoto wa mwanasiasa huyu aliyeishi Kenya na Marekani ktk maisha ya ufahari lakini akatumbukia ktk kujihusisha na biashara ya mihadharati Marekani alipokuwa anaishi pengine ili awaze kuendelea aina ya maisha ya ufahari alutimuliwa nchini Marekani na sasa anaishi maisha ya kusikitisha.
Peter Aloo Aringo Junior ni mtoto wa kwanza kwa wazazi wake Mzee Peter Oloo-Aringo na mama mwenye asili ya Jamaica. Oloo Junior alisomeshwa ktk shule za kifahari ghali nchini Kenya za Consolata Primary School ya Westlands Nairobi and St. Mary's Yala Kenya. Kisha St Patrick’s Iten alipomalizia A levels mwaka 1987. Baada ya kumaliza masomo ya upili, Wazazi wakampeleka nchini Marekani na kujiunga Chuo Kikuu cha Lona College akafuzu masomo ya shahada ya biashara na usanifu majengo. Alifanikiwa kupata kazi nzuri ya kipato nchini Marekani lakini tofauti ya kitamaduni /cultural shock alikuwa bado anayo alipoona waMexicana wanafanya biashara ya mihadharati bila woga na kutengeneza pesa nyingi.
Akiwa huko Marekani ndipo akaingia tamaa ya fedha nyingi na kuanza kuuza mihadharati. Hakujua alikuwa anafuatiliwa na idara ya upelelezi ya FBI ambapo hatimaye alikamatwa. Kortini akahukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya muda akapata bahati ya kutimuliwa (deportation) nchini Marekani kutokana na afya yake kuzorota gerezani Marekani na sasa yupo nyumbani Kenya sehemu za Nakuru west akiendelea na maisha kama mtu huru.
More info:
Soma historia ya mwanasiasa: Mzee Peter Castro Oloo Aringo : KENYA: WHAT HAPPENED TO THE DOZENS OF MOI ERA MADE LUO MILLIONAIRES ?