Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nakumbuka nilikuwa mdogo sana kiasi cha kushindwa kupambanua chochote katika yake ambayo yalikuwa yananizunguka.
Lakini nakumbuka ilikuwa katika miaka ya 1955 au 1956 niliposikia jina la mganga mfichua wachawi jina lake Nguvumali.
Huyu alikuwa akivuma katika midomo ya wazee wetu na kila mahali hadi sisi watoto tukawa jina hili limetukaa kabisa akilini.
Kifo chake kilipotokea katika ajali ya gari ndiyo kishindo kikawa kikubwa kabisa.
Nakumbuka sana historia hii kwa kuwa katika miaka hii mama yangu alikuwa mgonjwa na mimi nikawa nimepelekwa kwa mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha aliyekuwa anaishi Mtaa wa Narung’ombe na Nyamwezi karibu sana na Soko la Kariakoo.
Nyumba hii ilikuwa nyumba ya Mzee Kasembe mtu maarufu sana wakati wake kwani alikuwa karani bomani na bingwa sana wa kupiga taipu.
Enzi zile hii ilikuwa kazi ya maana sana.
Mzee Kasembe alikuwa na mwanae Richard ambae umri wake ulikuwa sawa na wangu.
Fikra zangu za awali za udogo wangu zikinijia Richard Kasembe lazima atanitokea.
Richard katangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita.
Nilisikia Nguvumali akielezwa kuwa alikuwa anakuja kutokea sehemu za Kilwa na basi na hilo basi limepata ajali njiani na Nguvumali juu ya uchawi wake hakuweza kujinusuru na amekufa.
Wazee wanasema Nguvumali alikuwa kabeba uchawi wake anakuja Dar es Salaam ili kumroga Julius Nyerere oil kudhoofisha harakati za TANU za kudai uhuru.
Kutokana na kifo hiki cha Nguvumali tafsiri nyingi zilitolewa wakati ule.
Pamoja na kisa hiki cha Mchawi Bobezi Nguvumali nina kumbukumbu za Boimanda.
Huyu Boimanda alikuwa mwendawazimu lakini hakuwa yule wa kuwadhuru watu.
Nakumbuka alikuwa na kofia yake kama ya trafiki aliyokuwa akivaa na matembezi yake sana ilikuwa pale sokoni Kariakoo na akipita nje ya nyumba yetu.
Watoto tulikuwa tukifanya utundu tunatishiwa kuitiwa Boimanda.
Ikawa watoto tukimuona Boimanda anakuja sote tunakimbilia ndani.
Boimanda alipigwa kichwa na mtu mmoja anaitwa Manyanga na akaanguka na kufa hapo hapo katikati ya soko.
Watu pale sokoni walikuwa na kawaida ya kumtania Boimanda kwa kumpigia kelele kumtisha kuwa wa kodi ya kichwa walikuwa wanakuja na yeye akisikia keleke zile za, ‘Kodi, kodi, kodi,’’ basi ataktoka mbio na ukiwa mbele yake atakuvaa akupige.
Wakati wa ukoloni kulikuwa na kodi ya kichwa na askari wakifanya msako kuwakamata wale ambao hawajalipa na kuwafikisha mahakamani n adhabu yake ilikuwa kufungwa jela.
Siku ile baada ya kusikia kelele za kodi katika kukimbia Boimanda akamvaa Manyanga kwenye ubao wake wa samaki.
Huyu Manyanga hili halikuwa jina lake jina lake ni Abdallah hili jina la ‘’Manyanga,’’ alilipata kwa kuwa baba yake alikuwa mganga wa kienyeji na katika kuagua kwake akipiga manyanga.
Hivi ndivyo huyu bwana alipozaliwa akakumbwa na jina hilo.
Hili tukio la kifo cha Boimanda lilikuwa tukio kubwa kiasi zilitoka khanga zenye jina la Boimanda.
Ukubwani nilikuja kufahamiana vizuri kabisa na kwa karibu sana na Manyanga lakini baada ya kujua kuwa kile kitendo cha yeye kumuua Boimanda kinamtia simanzi sana sikuweza kumuuliza ilikuwaje hadi akampiga kichwa Boimanda na kumuua.
Maisha yake yote Manyanga alikuwa akifanya biashara sokoni hapo Kariakoo akiuza samaki hadi alipofariki dunia.
Manyanga inasemekana hakufungwa kwa kosa lile is kuua bila kukusudia alikaa rumande kisha akaachiwa.
Wapo waliosema kuwa uganga wa baba yake wa kupiga manyanga ndiyo uliomnusuru.
Katika visa hivi viwili vya Nguvumali wasomaji wangu ndiyo watakaoamua kama Nguvumali alikufa kwa kutaka kumdhuru Mwalimu Nyerere au ahadi yake ilikuwa imetimia.
Halikadhalika wasomaji wangu ndiyo watakaoamua kama Manyanga alinusurika adhabu kwa kuua kwa uganga wa manyanga ya baba yake au kwa kuwa ilidhihirika kuwa hakukusudia kuua?
Miaka ile ya 1950 ushirikina ulikuwa umetamalaki sana katika jamii ya Waafrika si mijini wala mashambani.
Siku ya Jumapili Dar es Salaam ndiyo ilikuwa siku makhsusui ya mafundi kulisha viti vyao vyano, yaani kupunga majini.
Haya nayakumbuka vizuri kabisa kwani watoto tulikuwa hatuchezi mbali na pale mganga anapokuja kumpunga mteja wake kwa kuwa kile chano kilikuwa kinawekwa vitu vitamu kama tende, halua, sukari mawe nk na kile chano baada ya kiti kulishwa kidogo kidogo vilivyomo kwenye chano, kinachobakia chote tunapewa sisi watoto kula.
Itikadi yake ni kuwa vile vyakula vitamu anakula jini anaemtaabisha kiti kwa maradhi.
Haya mambo taratibu yakaanza kutoweka kwa kuja kwa uhuru na watu kuelimika na kujiweka mbali na mambo ya kishirikina.
Hivi sasa katika joto hili kali la siasa za upinzani ushirikina umerudi kwa kasi ya ajabu haba jana.
Waganga wamo katika ratiba ya safari ya viongozi wetu na wanatishia kuua wapinzani na kauli zao zinasambazwa kwa kasi kali ya ajabu katika mitandao ya kijamii watu wakisoma na kuona na picha, kusikia sauti na haya kuenea dunia nzima.
Dunia inashuhudia wataalamu wa "voodoo," katika mavazi yao rasmi ya ngozi, vibuyu na hirizi wakiwa jukwaa moja na wanasiasa wahitimu wa vyuo Vikuu vya Marekani na Uingereza.
Tumerudi nyuma tulikotoka nusu karne.
Taaluma ya Sangoma inachukua sura mpya ya kuheshika na kuaminika katika jamii.
Hii ni historia inajirudia na kuwa sehemu ya utamaduni wetu mpya au ni jambo la kupita?
Hivi wangapi wanajua kuwa kufanya uchawi ni kosa la jinai?
Au ni wangapi miongoni mwetu wanaojua historia ya Ton Ton Macoute wa Haiti ya Papa Doc?
Picha hii tulipelekwa kupigwa kwa Gomes studio maarufu Dar es Salaam miaka ile iliyokuwa Acacia Avenue (sasa Samora Avenue) katika kipindi hiki ninachohadithia baina ya 1955/56 na naikumbuka vizuri siku hii tunavishwa nguo kwenda studio na ndugu yangu Kapufi Yunge.
Mimi nilishikishwa kitabu ili nitulie ipigwe picha maana nilikuwa situlii kitini.
Picha hii ni moja ya ambazo mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed alinipa katika siku zake za mwisho za uhai wake akiniambia, ''Baba Mzee Mohamed picha zako hizi kaa nazo mwenyewe.''