Amani ya Mungu
Member
- Sep 1, 2011
- 45
- 70
Ukiachilia mbali kuwa Wilaya ya Manyoni kuna Kijiji kinaitwa Chisingisa ambapo ndio ipo alama ya kuonyesha pale ndio katikati kabisa ya Tanzania, lakini nimekutana na hichi kisa hivi karibuni. Pamoja na kwamba Manyoni ndio wilaya ya kwanza kabisa Kuongozwa Mkuu wa wilaya Mtanganyika mwaka 1958 aliyeitwa Dastan Omary naomba kushare nawe kisa hiki ambacho nimekutana nacho.
Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake aliwahi kufanya kisa kimoja ambacho pengine kinaweza kuingia katika Historia ya uhuru wa Tanzania Bara.
Wakati Mwalimu ana dhamira na msimamo mmoja tu wa kutaka Tanganyika ijitawale aliona wazi kuwa wazungu hawawezi kukubali na hivyo lolote linaweza kutokea hasa kwa nguvu kubwa waliyokuwa nao wazungu kwa kipindi kile. Akaamua Kabla ya kutangaza rasmi kuwa Tanganyika inataka kujitawala alirudi nyumbani kwao Butiama ili kwenda kuwaaga ndugu na majirani kuwa anakwenda Dar kwa ajili ya msimamo mmoja tu.
Hivyo ikamlazimu akakutane na makabila ya kwao mkoa wa Mara kama vile Wazanaki, wanyabasi, Wailege, Wanata, Wakurya nk. Na akawaambia kuwa Sasa nimeamua kwa dhati kwenda kudai uhuru na msiponiona tena mjue ndio nimekwenda (Wazungu wamemuua).
Wakati anakwenda Butiama alipita Manyoni, ambapo ilikuwa ni moja ya vituo vyenye wanachama wa TANU, akazungumza nao kuhusu safari yake ya kwenda kuaga hata hivyo hakuwaambia dhamira rasmi ya kwenda kuaga lakini wazee wa Manyoni walikuwa na shauku ya kutaka kujua lini atarudi. Na akawaambia atarudi tu, lengo lake kubwa ni kwenda kuitamka dhamira yake pale mnazi mmoja na yuko tayari kwa lolote litakalotokea baada ya kutamka dhamira hiyo.
Dhamira ya mwalimu Nyerere kuwa na kituo Manyoni ilijulikana kwa wazungu na wakajua kuwa atapanda treni ya kutoka Mwanza ili ashuke Manyoni na hivyo wazungu tayari walikuwa wamefika Mji wa Manyoni na Itigi kuhakikisha kuwa wanamkamata mwalimu kabla hajafika Dar es salaam. (ikumbukwe pia Manyoni kulikuwa na Jengo la Kiongozi wa Wazungu ambalo lipo mpaka leo)
Baada ya wazee wa Manyoni kuona ujio ule wa wazungu ukizidi mji mzima na mji jirani wa Itigi, ndipo wakajua kuwa wana lengo la kumkamata Mwalimu hivyo ikajitokeza timu ikiongozwa na Mzee Juma Kuwingwa, Hadj Omary na Selemani Matonya ambayo ikasema itamfuata mwalimu mpaka mji wa kaliua na Kusubiri treni ili wamtafute na kumueleza kinachoendelea Manyoni kabla hajafika, na waliondoka na vazi la kike aina ya baibi kwenda nalo Kaliua
Treni ilipofika Kaliua wazee wale waliingia na wakamtafuta na wakafanikiwa kumuona, na wakamwambia sisi ni watu wa Manyoni, tunakuteremsha ili dhamira uliyopanga kuitamka Mnazi mmoja ukaitamke Manyoni, sisi tutakulinda. Mzee mmojawapo aitwaye Selemani matonya akavaa baraghashia, akawa kama ndio mme wa mwalimu na Mwalimu akavalishwa baibui.
Wakati wazee hawa wamemfuata tayari kulikuwa na watu walioratibu raia kujikusanya mmojammoja kwenye nyumba ambayo walitaka Mwalimu afikie mule aweze kusema dhamira yake. Wajumbe walitumia siku nzima kuingia huku chakula kikipikwa ndani.
Wale wazee waliomfuata mwalimu wakaja na treni mpaka itigi, na muda huo wazungu wako chini wanaangalia kila anayeshuka, ndipo Selemani Matonya akiwa na bakora akateremka na mwalimu (akiwa kavaa baibui) kama mtu na mke wake huku wazungu wakiwa wamezubaa kumsubiri Mwalimu bila mafanikio.
Mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la mzee Mansoor akajitolea gari aina ya Ford wakawapokea Bwana na Bibi kuwapeleka mpaka Manyoni hata hivyo walipita njia ya kutokea Mkiwa ndipo wakaelekea Manyoni. Alipoingia ndani kwenye nyumba iliyoandaliwa na wakazi wa Manyoni mule ndani wakamwambia Tunaelewa wanakutafuta Tunachoomba utamke dhamira uliyopanga kuitamka Mnazi mmoja. Mwalimu akasema NAITAKA TANGANYIKA IWE HURU. Ndipo kikao kikaendelea mpaka saa 10 alfajiri ndipo wakamsindikiza kuondoka, lakini wakati wa kuondoka ilibidi asipite njia ya bahi to Dodoma, akapita njia ya kuzunguka kijiji cha Chikola mpaka mpakani mwa Dodoma na Manyoni kupitia upande wa Bihawana, na wakati huo wazee wale tayari walikuwa wamefanya mawasiliano na kina Malechela kutoka Dodoma na wakawa wameenda kumpokea Mpakani mwa Manyoni na Dodoma.
Kuna kila sababu ya kusema uhuru wa Tanganyika ulianzia Manyoni ukizingatia hata DC wa kwanza mtanganyika alianza kutawala wilaya ya Manyoni na yawezekana ndio ukawa mwanzo wa kuanza kujitawala mpaka kufikia kupata uhuru.
Mungu Ibariki Tanzania