Kisa cha rafiki yangu mpenda sifa.

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
Kila inapofika Mwezi Juni huwa nakikumbuka hiki kisa.
Rafki yangu aliniomba nimsindikize ukweni kwao ambapo mkewe alikuwa huko kwa ajili ya kusubiri tarehe ya kujifungua.
Tulipofika ukweni sasa.
Pale ukweni kwao palikuwa na mpera mferu sana na ulikuwa na mapera makubwa na mazuri.
Jamaa yangu bila kuombwa akadai anataka kumwangulia mkewe mapera.
Lakini baba mkwe wake akamsihi kutokana na mvua iliyonyesha siku ile isingekuwa busara kuparamia ule mpera.
Jamaa akamhakikishia baba mkwe kuwa pamoja na yote angepanda na angechuma mapera bila hatari yeyote.
Jamaa akapanda, akaangua mapera.
wakati wa kushuka bahati mbaya akateleza na kuanguka chini tena akafikia mgongo 'Pu!"
Wote tukastuka.
Rafki yangu hakubali kushindwa huku akiinuka na kujipukuta akatwambia ' Msiwe na hofu, ndo nnavyoshukaga hivi'
Siku iliyofuata sasa.
Kulikuwa na n'gombe ambaye wenyeji wetu humkamua maziwa.
Rafki yangu akaomba siku hiyo yeye ndo amkamue.
wenyeji wakamwonya wakamwabia huyo ng'ombe ni mkali, wakati wa kukamuliwa inabidi afungwe miguu.
Jamaa akadai yeye ana uzoefu na angeweza kumkamua bila kumfunga miguu.
Jamaa akaanza kumkamua.
Da! kilichotokea sasa...
Huwa nakumbuka kila inapofika tarehe kama ya leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…