Kisa cha 'Rubani Shujaa wa vita ya Uganda' kutapeliwa Almasi Tabora miaka ya 1980

Kisa cha 'Rubani Shujaa wa vita ya Uganda' kutapeliwa Almasi Tabora miaka ya 1980

Brothers Karamazov

Senior Member
Joined
Jul 13, 2023
Posts
152
Reaction score
393
Niko matembezini Tabora, kwenye kijiwe kimoja Nimekutana na Mzee mmoja mstaafu anaitwa Mzee Moshi, amenipa kisa kimoja.

Kuna Rubani shujaa sana wa kitanzania Brigedia Shimani (sina hakika kama jina nilimuelewa vyema). Huyu aliaangamiza wanajeshi wa Amini, kiasi cha kupongezwa kwa upekee na Mwalimu Nyerere.

Miaka ya 80, kuna mwamba akamfuata kambini kumuuzia Almasi, Shimani kazinunua.

Kwa muda wake akampelekea muhindi.. kaambiwa hizi ni chupa sio almasi. Chukua nyundo gonga, Zikavunjika.

Shimani akarudi kambini, na kisha kuelekea maeneo ya Ng'ambo kumsaka tapeli wake.

Kufika, mke anadai mmewe hayupo. Karudi tena baadae, hayupo. Akafupisha safari, Akalamba shaba mke na mtoto, na kurudi mes kula beer.

Police kutokana na cheo chake kijeshi, walishindwa hii kesi. Jeshi HQ wakamuita, kwa heshima yake walimuhifadhi huko.

Kwa mnaofahamu kisa hiki, huyu Rubani aliitwa nani? Yupo hai? Kesi ilimuandama ama ndio iliishia hewani?
 
Kwa mnaofahamu kisa hiki, huyu Rubani aliitwa nani? Yupo hai? Kesi ilimuandama ama ndio iliishia hewani?
Aliitwa Shimanyi, kanali wa jeshi, miongoni mwa marubani wa jeshi wa kwanza kusomea urubani Canada.

Hakuwa rubani wa ndege za kivita, alikuwa rubani wa ndege za jeshi za usafirishaji toka Canada tulizoziita Caribou.

Alihukumiwa kunyongwa, sina hakika kama alinyongwa au alifia jela.

Kwa umri kama atakuwa bado hai, atakuwa anakaribia miaka 90, my age mate.
 
Na ni kweli alipigana vita ya Uganda?
 
Hakupigana; vita ilianza akiwa tayari kishafanya majanga.
Nimekupata vyema. Asante sana.

Basi alinisimulia, hakuwa na kumbukumba sahihi ya matukio.

Hata hapo kwa usahihi haikuwa miaka ya 1980.

Pia sidhani kama alinyongwa, maana kumbukumbu zinaonyesha 'raia' aliyenyongwa ni yule wa Iringa, mwamwindi.
 
Back
Top Bottom