Kisa cha Zidane kulilia kwenda Juve, lakini anapokwenda anamkosa aliemfuata…

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Alipotakiwa na Juve Mwaka 1994 Zinedine Yazid Zidane alifurahi saana. Kisa cha yeye kufurahi ni kwamba angekwenda kuungana na Mchezaji wake boora wa muda wote ambae yeye anakiri kuwa vitu vingi alinakili kutoka kwake.

Lakini timu yake ya Bordeaux ilikataa katakata kumuuza kwa kauli kuwa wana mipango nae ya muda mrefu.

Zidane alikasirika saana na kuamua kuweka shinikizo kwa klabu yake kuwa iwe isiwe anataka kuondoka msimu ujao na kituo kinacho fuata ni KLabuni Juventus ili kwenda kukamilisha Ndoto yake.

Hatimae klabu ya Bourdeaux ilikubaliana na shinikizo hilo la Zizzou na Juve wakatenga kitita cha kumnyakua.

Katika bahati mbaya alizo wahi kukutana nazo Yazid ni kwamba wakati Juve wanatangaza kumnyakua kiungo huyo Mwaka 1996, yule role model wake alikuwa keshatimka klabuni hapo Mwaka 1995 na kwenda kukamilika klabuni AC Milan.

Zidane na Baggio hawakuwahi kucheza timu moja na ndicho kitu Zidane anakijutia maishani mwake.

Zizzou anatanabaisha kwamba katika maisha yake ya Soka alipenda saana kwenda kumkaba Baggio, na mara nyingi aliishia kudhalilika, lakini yeye anakiri kwamba kule kulikuwa ni kumjenga na sio kumdhalilisha.

Zidane anaweka wazi kuwa hata alipokuwa akifuatwa kukabwa na Zidane yeye alijisikia furaha saana kwa kuwa alikabwa na Mtu ambae amekamilika kila idara.

@gang_chomba🇰🇪
 

Attachments

  • IMG_9576.jpeg
    90.4 KB · Views: 7
  • IMG_9575.jpeg
    80.3 KB · Views: 8
  • IMG_9574.jpeg
    76.9 KB · Views: 7
Tamka zainadin yazid zaidan
 
Reactions: EEX
Lakini Italy kwa ujumla wake kipindi hicho kulikuwa na vyuma kwelikweli, ukisikia unaenda cheza na timu ya taifa ya Italy unajua kabisa unaenda kucheza na timu.
 
@Gang Chomba the legendary. Upo Mkuu?
 
BBwa
Kwa hiyo bwana Zidane alikuwa anajikaba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…