Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kisa hiki kinapatikana kwenye kitabu Unyonge wa Mwafrika.
Wakati mmoja nilipata kuwa Karani Mkuu wa Boma, wenyewe humwita Chief Clerk. Chief Clerk enzi za mkoloni mtu mkubwa sana. Ikafika sikukuu ya Malkia. Siku hiyo hualikwa machifu na watu wakubwa katika Wilaya nyumbani kwa D.C., kwa karamu ya chai kwa keki. Na mimi nikapata kadi. Bwana D.C. mwenyewe kenda livu kwao Uingereza. Wa chini yake Mwafrika, Kandambili, kaachiwa Boma kushika; na ndiye atakayeandaa karamu hiyo.
Basi ikawadia siku; tukajitia. Likapitishwa sinia la keki, kila mtu kachukactivat kipande. Kila mtu kesha wekewa kikombe chake, sasa anapita mpishi anatutilia chai. Kila atiapo kikombe hakijai; hufika shinda tu. Wote tunatamani vikombe vijae, lakini mahali pa watu wakubwa hatuwezi kusema. Ila mwenzetu mmoja hakuvumilia; mpishi anataka kuondoka kamvuta kanzu. "Nijazie." Akajaza mpaka kikombe kinafurika.
Kandambili kaja juu, anamgombeza mpishi, "Desturi gani hiyo, wastaarabu hawatii chai namna hiyo." Na mengine mengi yakamtoka, kutetea ustaarabu wa kizungu wa kunywa chai!
Wenye asili ya chai, China na Uhindi, hunywa chai baada ya kuipoza katika kisahani. Hiyo ndiyo asili yake. Wazungu hawawezi kufanya hivyo; kwao baridi. Hupenda wainywe chai ingali moto, iwapatie joto mwilini. Kwa hiyo hawathubutu kuipoza, wanapaswa kuinywa mle mle katika kikombe. Sasa wakinywa hivyo wazungu huwaletea matatizo. Pua zao ndefu mno. Kikombe kikijaa pua itaingia katika chai, na chai yenyewe ikiwa moto itamwunguza! Kwa hiyo ikawapasa wao vikombe vyao watie chai shinda. Kwa mzungu desturi hiyo ina sababu nzuri sana.
Sasa mwangalie Kandambili, Mbantu. Pua yake inchi moja, ikizidi sana inchi moja u-nusu; domo ndilo lililotokeza mbele. Hivyo ndivyo tulivyoumbwa. Kandambili naye akitetea ustaarabu wa Kizungu wa kutia chai kikombe shinda, hofu yake ni pua kuungua? Mzungu kasema chai hutiwa shinda, basi Kandambili naye anasema, "Chai hutiwa shinda."
Ndivyo tunavyoharibika mawazo yetu, tukasaidia bila kujua kueneza desturi na mila za kigeni kwa watoto wetu. Kila mila au desturi ina sababu zake; inafaa mahala pake. Lakini akina Kandambili ni wengi mno ambao wakiona kitu kafanya Mzungu, au Marekani, au Mhindi, hukikumbatia wakakifanya chao: wakati mwingine zaidi kuliko wenyewe. Mila na desturi zetu, zenye sababu za kikwetu zilizo nzuri sana, tunazitelekeza kwa sababu ya kukumbatia mno mila na desturi za kigeni.
Mwenezaji mkubwa wa mila na desturi hizo za kigeni, ambazo akina Kandambili wanazihusudu ni senema. Heri Kandambili, anatetea ustaarabu wa kunywa chai. Lakini tumeonyeshwa mambo mengi sana ya ovyo katika senema: pamoja na mini, na wig, na dawa za kuchuna ngozi. Wale walionaswa na maradhi hayo ukiwaambia kuwa wanaiga mambo ya ovyo utawasikia watetezi. Wengine watu wakubwa kama Kandambili, wanatetea kina mama kuvaa mini, maana inapendeza katika senema!
TANU imeutambua ugonjwa huo. Halmashauri ya TANU imeamua kwamba senema zetu zitengenezwe hapa hapa kwetu. Zitatengenezwa na sisi wenyewe, kwa faida zetu sisi wenyewe, ili kukamilisha juhudi yetu ya kuhifadhi zile mila zetu zilizo nzuri sana.
Chai ya Kandambili