Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nitag kwenye part 2 mkuu.
 
Hahahahah wajinga wanatembeza mkwanja hadi kwa polisi wa jirani na maeneo game lao lilipo ukienda ripoti polisi tu kama umeibiwa polisi anakuuliza 'ungekula au ungeshinda ungekuja?
 
Useless kabisaa nyie ndyo ambao mkiambiwa mkeo anatoka nje ya ndoa bila kutafuta ushaidi mnawaacha
 
Part 2

Siku ile baada ya kudhurumiwa niliumia saana sana hasa kwa kuwa hela haikuwa yangu pia hali ya uchumi mtaani kugumu. Basi bwana, kufika jioni dogo akanichek kupata mrejesho wa betri lake, ikabidi nimwambie yule jamaa kafunga kaenda msibani so atarud after siku tatu na kununua sehemu nyingine ni bei sana. Nashukuru dogo alinielewa japo kishingo upande.

Ishu ya kudhurumiwa iliniima saana sanaa sana ilifika kipindi nipo busy na mambo mengine lakini moyoni unakuwa kama kuna kitu hvi hakiko sawa ukikumbuka unagundua hela yako imeenda kiboya. Hivo nkapanga mikakati narudishaje pesa yangu niliyodhurumiwa hadi kwa wakati ule usiku sikujua nn ntafanya.

Kesho yake mchana nkapada gari hadi pale pale kwa wachezesha bahati nasibu, lengo lilikuwa niende nisome mazingira tena nimezurumiwaje kiboya vile tena laki. Laki yangu ilikuwa inaniuma kinoma na isitoshe nimemdanganya dogo so baada ya siku tatu anategemea nimtumie betri lake na isitoshe dogo ananiamini kinoma.nilishukia kituo kinaitwa pamba road sheli. Mdogo mdogo hadi pale kufika tu pale nkasimama kuchek wahusika nkakuta yule mdada aliyeshinda begi ndo anagawa tiket yule niliyechanga nae hela ni msaidizi ndo nkagundua huu ni mchezo hakuna bahati nasibu wala nini hapa, kuwaona pale kichwa kikazidi kujaa sumu. Wale watu bhana kumbe wana mabaunsa nkaona hapa nkileta fujo ntajikuta nipo polisi so nikawa mpole. Sasa kumbe yule mdada tuliyechanga nae hela alinijua akasema kwa nguvu "kuna wengine wamerudi kufanya fujo baada ya kuliwa jana" basi mabaunsa wakaja wakanifukuza baada ya kuoneshwa kuwa ni mimi na isitoshe ni kweli jana nilitaka kufanya fujo baada ya kudhurumiwa. Nkajua hapa kitumbua kishaingia mchanga, wakanifukuza pale nkatoka lakini nikawa najua mchawi wangu ni yupi ni yule dada aliyenichongea kwa mabaunsa.

Nkatoka pale nmejaa sumu kinoma, nkaenda zangu kamanga "Bismark rock" kuna kabustani pale kwa wenyeji wa mwanza washapafahamu, nkalipia jero nkakakaa kwenye nyasi napunga upepo wa ziwa huku natafakari nini cha kufanya.

Kichwani likaja wazo nilisema nipambane nao siwawezi kwanza wana mabaunsa, niende polisi siwezi, inamaana polisi hawajui kuwa hawa jamaa ni matapeli? Nkajisemea hapa nadeal na huyu mdada aliyenichongea anajifanya mwema kumbe ni snichi. Sasa ikawa muda wa kupanga mikakati namna ya kurudisha pesa yangu.

Njia ya kwanza nkawaza nimvamie nimnyang'anye simu na hela nkaona ntaitiwa mwizi nkasema hapa lazima nijue anakaa wapi kwanza ndipo mambo mengine yaendelee.

Sasa baada ya kurudi home ilikuwa mwanzo wa mwezi na mimi ndo nakusanya hela ya maji, tunapokaa tupo wapangaji wengi kidogo, nkakusanya hela ya maji kama laki na 30 hvi nkaenda kulipa 60 na 70 nkanunua betri la dogo nkamtumia. Nkachonga na jamaa anaekujaga kukata maji kama hujamaliza deni coz tulikuwa tunafahamiana nae kiasi na namba zake nilikua nazo coz kuna msala ashawahi nisaidia, nkamuahidi baada ya wiki mbili hvi ntakuwa nshamaliza deni so likitokea lolote anisitiri coz wapangaji wenzangu wanajua bill ishalipwa yote.

Nkapanga mikakati, mkakati wa kwaza ni kubadili mwonekano ili nikirudi pale nisijulikane kirahisi, hivo nilienda kunyoa nyele zoote na ndevu yaani full para coz nilikua na nyele ndefu na madevu mengi. Kiukweli nilibadilika saana hadi demu wangu alisema hajazoea kuniona vile, pia washkaji wengine walinisahau kabisa, nilifanya hvi ili nisigundulike hata nikimfatilia yule dada anapokaa hata tukipanda daladala moja asihisi chochote.

Katika maisha mimi huwa naamini kuwa tunaishi mara moja tu so ninachoamini, jambo likiumiza kama umeamua kusamehe basi samehe kama kulipiza kisasi, lipiza coz maisha ni kma maji yanayo toka mlimani kwenda bondeni yakipita hayarudi tena kwa kifupi tunaishi mara moja tu, punguza majuto katika maisha. falsafa hii ndio chanzo cha kujiita "MTAMAUSHI" kwa waliosoma somo la kiswahili vizuri levo ya chuo na advance wanaelewa nini maana ya falsaha hii ya ndugu E kezilahabi kma sijakosea.

Tuachane na falsafa, baada ya kubadili mwonekano nkarudi tena pale pale kwa wanapochezesha bahati nasibu lakini awamu hii nilirudi jioni saa 10:30. Nilikaa pembeni kidogo walikua wanakaanga chipsi, nkaagiza chipsi na soda nikawa nakula taratibu nkivizia wafunge. Baada ya kumaliza kula nkaagiza soda nyingine nkaanza kunywa taratibu, kweli bhana saa 11: 30 hvi wakawa wamefunga wanakusanya kila kitu pale wakakutana pembeni kama kimduala hvi wakagawana hela ndo nilipojua kumbe wanapiga mkwanja mrefu. Hela alikuwa anagawa kiongozi wao, baada ya kugawana wakaanza kusepa wengine kwenye gari lililobeba vyombo wengine kwa miguu, target yangu ilikua ni yuje mdada tu. Akatoka pale mdogo mdogo akaingia sokoni mimi nyuma yake ila kwa mbali na umakini mkubwa sana asijue lolote. Yule dada alinunua vitu vichache pele akaenda kupanda gari. Baada ya kufika kwenye gari alikaa siti ya mbele kwa dereva nilichofurahi ni kwamba alikuwa kumbe anakaa njia ambayo namimi naishi huko hvo alinipunguzia garama ya usafiri coz niliapa kokote anakokaa nitamfata tu. Basi bhana baada ya abiria kujaa nkajisogeza pale nikakaa ndani ya daladala gari likaondoka likapita kituo ninachoshukiaga mimi hadi kama vituo 5 mbele yule dada akashuka. mimi sikushuka, gari lilipoanza kuondoka limetembea mita chache nkamwambia konda anishushe nilikua nimejisahau kweli nilishushwa ila kwa matusi na misonyo kibao ya konda kwamba sipo makini kumbe nilipanga iwe hvo. Baada ya kushuka tu nilianza kwenda kituoni kumchek yule dada, nikamwona kwa mbali anatembea. Nilikua nmevaa sweta jeusi nikavua nkabaki na shati tu nilifanya hvo asikumbuke kama tumepanda wote daladala kama aliniona. nilimfatilia hadi anapokaa nkapajua uzuri nyumba ilikua imejitenda kidogo na njia ina kichaka na uchochoro kidogo.

Baada ya kujua anapokaa nilirudi zangu geto kusubiri nifanye revange yangu, baada ya siku kadhaa saa 12:00 nipo kituoni namsubiri mfukoni nina bonge la panga. Saa moja na dk kadhaa nkamwona kashuka nikatangulia mbele coz yeye alipita kununua mhindi choma pale standi. Kwa wakati ule nilikua nakumbuka ile kauli yake ya "kuna wengine wamerudi kufanya fujo baada ya kuliwa" hii kauli iliniuma sana. Sikuwa na lengo la kumdhuru ila tu nirudishe hela yangu tu.

Baada ya kutangulia mbele nnkaanza kutudi nilikotoka tukakutana jiani nkachomoa panga. Nkamwambia naomba hela zangu, akauliza hela ipi? nilimpa ubapa wa mgongoni nkamwambia ukipiga kelele umekwisha, alitetemeka yule dada sijapata ona. nkamwambia leo nimekufata na huku mnapenda kudhurumu watu mbwa nyie. lete mkoba akawa anabisha nkampa bapa la pili akaachia nkazama kwenye mkona nkatoa simu na hela nkasepa zangu mbio uchochoroni nkamwacha anali na isitoshe watu hawakuwepo .Njiani nkadaka boda hadi karibu na geto nkashuka. Nilipofika home kuhesabu nkakuta hela kma 70 hvi simu, nkawafata wahuni kesho yake nkawauzia kama 50 ilikua smartphone. Nkalipa deni la maji na usumbufu.

Inayofuata:
Fema club walisababisha nikamatwe na bro nikiwa napiga punyeto kisa ile kauli yao ya punyeto ni njia salama, ntawalete kisa soon
 
Umetisha sana mkuu, mie pia napenda sana kulipa visasi.
 
Naisubiria kwa hamu na hiyo nyingine
 
Uzi unafurahisha sana,

mtamaushi ulifanya poa kurudisha pesa zako, ulimpa fundisho huyo dada,
 
Wewe ni mwamba ,hongera sana
 
Kuna kipindi nilikuwa nafuatilia FAO LA kukosa kazi Kibaha PSSF,nikawasiliana na sister mmoja akanambia Kuna mtu anaitwa Mohamed Chawa nimpigie anaweza kunisaidia kuzipata.Jamaa akahoji ni sh ngapi nilipotata milioni kadhaa yeye akadakia ni kweli akaongeza na Malaki kadhaa,nikajua hapa nimepata mpunga wangu.Akanambia niandae laki ya kumpa mhasibu halafu kesho yake nifuate check yangu.Machale yalinicheza aliposema niwekee kwenye tigo pesa kabisa halafu niende ofisini,nikaweka ila sikutaka kutuma hadi niingie ndani niangalie situation.Wakati nakaribia kuingia nikaone nisije kuharibu nikamtumia nikaingia ndani.Yule bwana Chawa akanambia ingia Kaa subiri.Ghafla akapiga akanambia niongeze 27,500 nikamwambia Sina akasema sawa.Baada ya dakika kadhaa namba haipatikani.Ikabidi niulizie kwa wamama wa pale ofisini,wakastuka wakasema umetapeliwa.Wakadai huyo mtu wanamtafuta,ikabidi twende polisi Kitengo cha Cyber,baada nikaona polisi watataka pesa nikamwambia basi ngoja nifanye nimetoa sadaka.Mohamed Chawa kama upo hai,niombe msamaha au shupaa uviko 19 iondoke na Wewe.
 
Haya matukio yalinikuta Sana,nyumbani kwa afisa wa JWTZ Tandika .Dogo akinificha Sana boys quarter uvunguni.
 
Visa vyenu kama vyangu sema Mimi nilikuwa naiba kweli.Darasa la tatu nilifiwa na kaka yangu ,shuleni wakanichangia nikala zikaisha nikaunga kwa Mzee nilipogundua anapoficha pesa zake.Mzee alipostuka akaanza uchunguzi kwa wanafunzi wenzangu na nilikuwa nikinunua vitu siwapi,nikila na mademu tu.Jamaa wakataja kila kitu.Jioni nilipomuona Mzee na bi mkubwa wamekaa wanahesabu pesa nikajua Leo ndo Leo.Baadaye nikaitwa kikaanza kipigo,nilitundikwa kama komando Lijenje na lingw'enya.Wadogo zangu wakaanza kilio.Nilipigwa hadi Mikono ikafa ganzi,walinitundika Kwa mpira yaani ,mnati.Baada ya hapo habari zikasambaa shule,mtaani na kila ndugu akija home anapewa story nzima,nikimgusa mdogo wangu Hilo ndo tusi.Kuna siku nilichukua dumu la sumu niinywe ,nife lakini Roho wa Mungu akanizuia.Hapo nilikuwa nimefumaniwa siku ya open day.Matukio hayo yalijirudia Sana hadi nikatamani niache shule niondoke home.
 
Siku niliyokamatwa napiga punyeto na bro:

Wakati nipo shule o-kevel hakuna kitu nilikua nakichukia kama club za masomo. Nakumbuka ilikua kila alhamisi, kilichokuwa kinanifanya nisipende ni maswali mengi kutoka kwa walimu na viongozi wa club husika yaani unapigwa maswali mbele ya madogo na ukikosea kujibu full aibu.
Basi wakulungwa wengi tulikua tunajazana kwenye club za michezo na fema. Mimi nilikua napenda fema coz ya mada nyingi ni za ujana. kule ndo nilipopata ujuzi wa kupiga punyeto. Wale jamaa walikuwa wanagawa na magazeti yao ambayo ndani wanasema njia mojawapo ya kujikinga na ukimwi ni ngono salama mojawapo ni punyeto a.k.a. selfee.

Basi bwana nilikua na mshkaji wangu anaitwa yaseen, huyu bwana anajua stye zote za punyeto na utamu wake, mara akwambie nyingine unapita mkao wa kukata gogo, nyingine unapiga umelala chali na ukikaribia kumwaga unapanua miguu unaanza upya. Hizi style zake zilinikosha kinoma. Huyu bwana alitoa ahadi siku akija kununua pc kitu cha kwanza atajaza video za x mtupu coz ndo starehe yake. Sitasahau kuna siku alikuja geto kuchek x kwenye pc ya bro mvua ikaanza kunyesha akalazimika kutoka hvohvo na mvua kisa anawahi kudowload ( kukumbuka) kabla muda haujapita ili asisahau akadai ili punyeto iwe tamu.

Kupitia huyu jamaa ndio nilikuja kujua kuwa kuna mshkaji wetu alikua mtu wa dini kinoma tena kiongozi alipiga punyeto getoni kwake akazimia akakutwa na bro ake hajitambui, nilicheka kinoma, huyu jamaa tulizoea kumwita kakoba coz alifanana sana na mshkaji mmoja kwenye maigizo ya ITV ya kila jmoc usiku alikuwa anaitwa mjomba kakoba.

Pole pole na mimi nikaanza huu mchezo wa punyeto na full kuapply style za mskaji wangu yaseen the master. Siku zote nilizoea kupigia bafuni, nilikua na mtindo wa kuoga maji ya moto hata kama ni mchana, nyumbani walinishangaa kinoma, kumbe mimi nilikua na lengo langu. Maji ya moto nilikua nayamwagilizia pale nnapokaribia kupiga bao + na lile joto la maji raha yake sio ya nchi hii. Hii style alinipa master wangu yaseen.

Basi bhwana chumbani nilikua nalala na bro sasa kuna siku bro alisema anaenda town nkakumbuka ndo mida sahihi ya kupiga puli coz pc ameiacha. Nkachukua cd yagu ya pilau nkaiweka nkaanza kuangalia baada ya mzuka kupanda nkachukua mafuta nkapaka kwenye mashine nkaanza taratibu kupiga punyeto, nilipata ujasiri wa punyeto ni salama hasa baada ya kushauriwa na fema club shuleni. Sasa ile utamu umekolea mara bro huyu hapa karud gafla na isitoshe mlango sikuufuga, aisee nilistuka balaa nachanganyikiwa nishike kipo nivae nguo coz nilivua zote au nizime pic, so nkabaki tu nimeduwaa sijui la kufanya. Daaah bro alimaind kinoma na isitoshe alikua ananiamini kinoma kila siku ananiona sio mtu wa mambo hayo . Bro ikabid aanze kunishauri kila siku kuwa mchezo huo sio mzuri. Moyoni nilimlaumu sana jamaa yangu yaseen coz alichangia pakubwa kwa mimi kuwa mpiga punyeto maarufu.

Kisa kinachofuata:
nilinusurika kufumaniwa na baba wakati nafanya mapenzi na beki tatu jikoni. Kalituona kadogo kamoja kakaja kusema sebuleni.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Daah pole sana aisee
 
salute mkuu unafaa sana kuwa kachero sijui kwa nini watu kama nyie hawawaoni asee
 
Mkuu ile hela ininiuma kinomaaa sikuwa na namna zaid ya kufanya mbinu za kuirudisha
Kama hukumtoa roho mi naona uko sahihi, kwani yako so alifurahia Basi ndo maumivu yake hayo, tena ingependeza ungepata hata laki zako 2 hivi au 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…