Kisa Milioni 6, Mtendaji wa kata akutwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na kifungo cha miaka 20 jela!

Kisa Milioni 6, Mtendaji wa kata akutwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na kifungo cha miaka 20 jela!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani Songwe imemhukumu kifungo cha miaka 20 gerezani aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbuyuni baada ya kumkuta na hatia ya uhujumu uchumi.

Afisa Mtendaji huyo, Assan Jacob anadaiwa kukusanya Shilingi milioni sita kutoka kwa wananchi 200 wa kata hiyo kwa ahadi ya kuwasaidia kuwekewa umeme wa REA kisha kuzitumia pesa hizo kwa mahitaji binafsi.

Kina Mengele, Abdul, wasanii, wanatimba mamilioni bila jasho!
Bongo kweli kujuana tu!
 
Kuna watu watasema mbona vigogo wanaachwa, lakini jiulize mtu wanaachi wanaolipa elfu 27 uwatoze watu 200 je kawaumiza kiasi gani?
 
Mnapena kazi kindugundugu mtu ofisi ya serikali anaona km duka la Baba yake anajichukulia tu anachojisikia si anajua kikibuma atapata backup ya Mzee
 
Wakuu,

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani Songwe imemhukumu kifungo cha miaka 20 gerezani aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbuyuni baada ya kumkuta na hatia ya uhujumu uchumi.

Afisa Mtendaji huyo, Assan Jacob anadaiwa kukusanya Shilingi milioni sita kutoka kwa wananchi 200 wa kata hiyo kwa ahadi ya kuwasaidia kuwekewa umeme wa REA kisha kuzitumia pesa hizo kwa mahitaji binafsi.

Huyu hakuwapa mgao wenzake.
 
Kweli amekiuka maadili ya utumishi na ni kosa la jinai, ila miaka 20 😳😳😳😔
 
Kashindwa kuelewa codes za kula kwa urefu wa kamba.
 
Hii Takururu inawafunga na kupambana na vidagaa huku ikiwaacha mafisadi papa.
 
Back
Top Bottom