Kisarawe: Mwananchi adaiwa kupokwa ardhi kwa nguvu na kubambikiwa kesi za jinai ikiwemo mauaji

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Makala iliyochapishwa na Watetezi Tv inamuonesha Mwananchi huyo Athuman Mohammed Zuberi (46) na baadhi ya wanafamilia wakieleza madai mbalimbali wanayodai kukumbana nayo.👇

View: https://youtu.be/sr_GveiZRys?si=475ZvP2mAA27aQ0c

Wakili Olengurumwa anatoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini kumulika suala hilo

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za BInadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa ameitolea wito Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini kuingilia kati na kuchunguza Sakata la Mkazi wa Kijiji cha Gwata wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani anayedaiwa kuondolewa kwa nguvu kwenye nyumba yake na kisha kubomolewa.

Akizungumza na Watetezi tv , Wakili Olengurumwa amesema kinachofanyika kwa mkazi huyo Athuman Mohammed Zuberi (46) ni kinyume na Haki za Binadamu na Utawalabora kwakuwa amekuwa akitishiwa Maisha na kufunguliwa kesi mbalimbali ili aache kudai nyumba yake na ardhi.

Habari zaidi zinasema Mkazi huyo alikabidhiwa ardhi ya Hekari ishirini na viongozi wa Kijiji hicho kwa ajili ya makazi yake mnamo mwaka 2012 kabla ya kuanza kukumbwa na misukosuko akitakiwa kuondoka kwenye eneo hilo .

“ Bwana huyu amenyanyaswa sana amefunguliwa kesi za kubambikiwa,kesi za mauaji,amefunguliwa kesi mbalimbali amewekwa ndani ye na mtoto wake, ofisi yangu ya Uwakili imeweza kumsaidia bure,kuhakikisha zile kesi anazipangua na leo mnamuona yuko hapa” Amesema Olengurumwa

“ Hata kama kweli lile eneo ni la kijijiji ,waliompa lile eneo ni viongozi wa Kijiji,ungefanyika utaratibu na busara walau aachiwe hata nusu heka ,hata Heka moja kwa ajili ya kusitiri na kuendelea kuitunza familia yake” ameongeza Olengurumwa.

“Naiomba Tume ya Haki za BInadamu,na nimeshaongea na Tume ya Haki za Binadamu,iende ikafanye uchunguzi juu ya suala la huyu Bwana katika wilaya ya Kisarawe,kuangalia kwamba Haki ya huyu haipotei” ameongeza Olengurumwa.

Jitihada za kumtafuta mkuu wa wilaya hiyo zinaendelea ili kuzungumzia shutma hizi.

Source : Watetezi tv
 
Attachments

  • VID-20250113-WA0022.mp4
    13.3 MB
Hii ndio Tanganyika watauza hadi watoto wetu.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom