Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Mtawala wa Rumi Julius Ceasar aliwahi kukamatwa kama mateka na maharamia. Wakamshikilia na kudai walipwe vipande vya shaba 20,000 ambazo ni sawa na Pound 500,000 za leo.
Ceasar akaona hii dharau mbona wanadai malipo madogo mimi sina thamani ndogo kiasi hicho. Akawambia wadai vipande vya shamba 50,000 ili kuendana na thamani yake.
Basi wale maharamia wakadai kiasi alichotaka.
Ceasar kwa kiburi alichokuwa nacho, kwa muda wote huo hakukubali kuwa yeye ni mateka bali alitaka awe kiongozi juu yao.
Akiwa kwenye chumba ndani ya meli ya maharamia, aliwazuia wasiwr wanapiga kelele akiwa kalala. Pia alitumia muda mwingi kuandika hotuba na kutunga mashairi ambapo aliwalazimisha kukaa na kumsikiliza akisoma hotuba alizoandika na kuimba mashairi, nao bila hiyana walitii.
Alianza kuwa anawaagiza na kuwapa kazi kama vile yeye ndiye kiongozi wao.
Baada ya muda wakawa kama marafiki akawa anafanya nachotaka wala hakuna anayemfuatilia.
Ikafika muda meli ilipokuwa ikitia nanga bandarini alikuwa anaweza kwenda kokote atakapo kisha akarudi.
Ila Ceasar alikuwa akiwambia kuwa madai yao yakishatimizwa akaachiwa, wakae wakijua kuwa atawatafuta kila pembe ya dunia na kuwaua kisha kuwatundika msalabani.
Kutokana na kuzoeana na ule urafiki waliokuwa nao kwa kipindi walichokaa nae, walidhanj jamaa hawezi kuwa serious.
Basi, hao maharamia wakalipwa, Ceaser akaachiwa akaondoka.
Haukupita muda akarudi na jeshi lake akawakuta pale pale, akawakamata na kuwachinja kisha mili yao kuitundika kwenye miti.
Huyo ndiye bwana Ceaser....