Kisheria inakuwaje mtuhumiwa akileta ushahidi wa kughushi, naweza nikamfungulia lingine?

Kisheria inakuwaje mtuhumiwa akileta ushahidi wa kughushi, naweza nikamfungulia lingine?

Joined
May 19, 2023
Posts
20
Reaction score
34
Naulizia, inakuwaje kisheria kama Mtuhumiwa amewasilisha hati ya ushahidi iliyoghushiwa, Mbali na kuikataa isitumike, Je naweza nikafungua Shauri jingine dhidi yake Kwa kughushi nyaraka?
 
Naulizia, inakuwaje kisheria kama Mtuhumiwa amewasilisha hati ya ushahidi iliyoghushiwa, Mbali na kuikataa isitumike, Je naweza nikafungua Shauri jingine dhidi yake Kwa kughushi nyaraka?
Kabla ya kuwasilisha ushahidi wake mbele ya mahakama huapa kwamba atasema kweli.. Kweli tupu! Hivyo akileta ushahidi bandia hiyo ni kesi nyingine
 
Kabla ya kuwasilisha ushahidi wake mbele ya mahakama huapa kwamba atasema kweli.. Kweli tupu! Hivyo akileta ushahidi bandia hiyo ni kesi nyingine
Sawa, hivyo naweza fungua madai mengine kutokana na tukio Hilo na likawa na hukumu yake inayojijegemea ?
 
hivyo naweza fungua madai mengine kutokana na tukio Hilo
Kugushi nyaraka ni kosa la jinai na sio madai, kwaio ukitaka kumfungulia kesi uende polisi na sio hapo mahakamani.

Ushauri wangu, kama kagushi ushaidi na mahakama imesha ukataa, basi wewe endelea tu kudeal nae na hiyo kesi yako ya madai. Mbali na kwamba kumfungulia jinai inaweza tafsirika kama chuki dhidi yake, lakini pia unaweza ukajikuta na wewe pia unajipotezea muda mwenyewe.​
 
Acha roho mbaya mleta mada ,dili na kitu kimoja sasa unataka asitafute namna ya kujinasua ,una roho mbaya sana na unapenda kesi ,natumaini hata maendeleo wewe huna kabisa
 
Naulizia, inakuwaje kisheria kama Mtuhumiwa amewasilisha hati ya ushahidi iliyoghushiwa, Mbali na kuikataa isitumike, Je naweza nikafungua Shauri jingine dhidi yake Kwa kughushi nyaraka?
To file forged documents in court is unacceptable. In the case of Mohamed Athumani Bado Vs Leila Kalebu Makundi Misc Civil, Application No 14 of 2022, HC at Temeke, it was stated that; ''I wish to comment on allegedly forged documents.Filing forged documents in court is unacceptable. Lying under oath is detestable by any standard...."
 
Back
Top Bottom