Kisheria ipoje? Deni au wizi wa kuaminika?

Kisheria ipoje? Deni au wizi wa kuaminika?

Bingili

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
310
Reaction score
799
Kuna jamaa yangu kabisa tunafanya biashara moja kwa hiyo huwa tuna aminiana anaweza kunipa mzigo niende kumuuzia au kumnunulia na pia mimi nampa pia

Mwaka jana mwezi wa 5 nikampa mzigo wa kama M6 akauze, akauza mzigo na tukawasiliana kwamba atanitumia hela kesho, kesho akaleta hadithi.

Hadithi zikaendele hadi wiki 3 baada ya hapo akawa hapoke simu na baadae akapotea hewani
Akaja kuibuka mwezi wa 10 akadai alipata dili akaona atie hela zote huko maana lilikua lina lipa lakini akapigwa
Akadai atanilipa kila mwezi M1 nikamkubalia sababu ni jamaa yangu na ikabidi tuandikishiane akiri kwamba namdai hela zangu na alizitumia kimako na yupo tayari kulipa M1 kila mwezi

Toka mwezi huo wa 10 jamaa hajanipa hata shilingi ni sound tu kila siku, mjumbe akapendekeza nimpeleke mahakamani.

Jamaa naye akaanza kiburi oooh usipelekeshe deni halifungi mtu nipeleke popote hata mahakamani nitasema uwezo wangu ni kulipa 10k kwa mwezi

Sasa huyu mwamba katangaza vita na mimi hatakikulipa deni nimpeleke mahakani

Swali langu

Siwezi kumfungulia kesi ya wizi wa kuaminika?

Kwamba huyu ni tapeli tu kanitapeli hela zangu kinyume na makubaliano

Nimeamua kuachana na deni ikibidi ili dili na wizi

NB: Maandishi mbele ya mjume kuwa namdai aliandika kwa mkono wake. Nina sms zake na voice note ambazo zina majibizano yote nilikuo nampigia baada ya kuona anaanza kuniletea hadithi

Naomba ushauri wenu
 
Watu wamekua siyo waaminifu,bora kumpeleka mtu polisi kwa kesi ya wizi wa kuaminika,then mtaenda mkaongee mahakamani kama atachomoa na kugeuka kua ya madai.
 
Kuna jamaa yangu kabisa tunafanya biashara moja kwa hiyo huwa tuna aminiana anaweza kunipa mzigo niende kumuuzia au kumnunulia na pia mimi nampa pia....
Ukilalamika na kumfungulia kesi ya jinai (wizi wa kuaminiwa) itakuongezea mzunguko mrefu. maana utapaswa kusubiri kesi ya jinai iishe then ukishinda uje utumie hukumu hio kama sehemu ya ushahidi kwenye madai

hapo muhimu fungua madai ili mmalizane mapema uzuri ushahidi upo
 
Back
Top Bottom