Kwakua kopi orijn anayo warioba ccm wamekwisha
JF bana!, kila mtu ni mwanasheria!, ana uwezo wa kutafsiri sheria!.
Issue nyingine jape simple ni too tenchical kwa asiye mtaalamu!.
Uhalali wa katiba, utatokana na wananchi!. Watu waliopewa mandate na wananchi, ni wabunge wa bunge la katiba na sio Tume ya Warioba!.
Kazi ya tume ilikuwa ni kukusanya tuu maoni, ya wananchi, wawakilishi wao ndio wenye uamuzi wa mwisho!.
This is the situation!.
Sherehe ya harusi (katiba) inaandaliwa, kamati ya maandalizi inatumwa kuwauliza waalikwa watapenda kula nini?.
Kuna watakaopenda kula ugali, "serikali moja", kuna watakaopenda kula pilau "serikali mbili" na kuna watakaopenda kula biriani "serikali tatu!".
Kamati inaamua kufuatia wapenzi wa biriani kuwa wengi, kamati inaamua chakula cha harusi ni biriani!, "wengi wape!".
Kumbe "Bwana Harusi" anapenda pilau!, hivyo anaamua kuwaelekeza wapishi waandae pia mapishi ya pilau na hata ugali!.
Siku ya harusi imefika, chef (bunge la katiba) anarudi kwa mara ya mwisho kuhakiki kinapikwa nini kati ya ugali, biriani na pilau, ndipo bwana harusi anawauliza hao wageni wanapenda nini, wengi kwa sauti moja wanaitikia "pilau!", Bwana harusi anamwambia chef apike pilau!. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, hawezi tena kupinga eti pilau isipikwe kwa sababu mwanzo walio wengi walichagua biriani!.
Uamuzi wa wajumbe wa tume ya katiba walio wengi ndio final na sio mapendekezo ya tume ya Warioba!. Ya Warioba ni mapendekezo tuu yanaweza kukubaliwa, kurekebishwa, kuboreshwa au kukataliwa!.
Pasco.
Mkuu Gisana, hoja yangu ni haws wafasiri wa sheria wasiojua who is mightier kati ya tume na bunge la katiba!. Wanadhani maoni ya tume ndio ya mwisho na bunge la katiba ni just a rubber stamp kuyapitisha hivyo hivyo yalivyo!.MKUU kwani ni kosa kila mtu kuwa mwanasheria? sheria zenyewe zinasema....ignorance of law is not a defence, ....unless the ignorance itself is a subject matter of the offence under question in that particula proceeding.
Leo nilikuwepo Mjini Arusha na Nimemsikiliza kwa Makini sana Judge na Pastor wangu Augustine Ramadhani, ameongea kisheria zaidi sio kisiasa wala Kiharakati.
Bunge lina mamlaka kisheria kutunga sheria na kubadili Rasimu ya Katiba bila ya kuwekewa Limitation kwa kuwa lina
' Legitimacy Power' kutoka kwa wananchi Directly na ndio maana hata hawa wajumbe 201 wa kuteuliwa hawawezi kudilute legitimacy power ya Wabunge wa kuchaguliuwa na wananchi., tume ya Warioba iliteuliwa na Mtu mmoja tu ( Rais wa Jamhuri) tena bila ya kuwepo sheria na kanuni za msingi zenye uwezo wa Ku Over power mamlaka ya Bunge.
Taasisi gani au mamlaka gani huru iliyosimamia ukusanyaji wa maoni katika tume hiyo kiasi cha kuamini Takwimu za kusema asilimia fulani ilitaka jambo gani? Tume ya Warioba yenyewe imekusanya maoni, yenyewe imehariri, yenyewe imeandika Rasimu, halafu Tuipe Mamlaka ya kulizidi wabunge wakati hawa ni wateule tu wa Mh. Rais ambao hatujui legacy yao kwa wananchi. Pengine tungeomba ridhaa ya wananchi kupewa ujumbe wa tume pengine wote wangekataliwa.
Nani anaweza kututhibitishia hapa kuwa Warioba na Tume yake wana Legitimacy ya wananchi
Upo sawa kwa upande flan lakin tambua kua hao wabunge wenye "Legitimacy power" ndio walio pitisha hiyo sheria inayo wazuia wao kubadir rasimu, kinyume na hapo watakua wameivunja sheria walio itunga wenyewe.
Ulitaka Warioba atunge na kupitisha sheria za nchi ? Chombo chenye mamlaka ya kupitisha sheria ni bunge.Sasa bunge la nini?
haijulikani maana waandishi wote wa habari wametimuliwa huko.