Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
Na Debora C. Kiyuga✍🏽
Katika kipindi cha Serikali ya Magufuli, vimejengwa viwanda vipya 8,477, ambapo vikubwa ni 201, vya kati 460, vidogo 3,406, na vidogo sana 4,410. Hii imeongeza idadi ya viwanda nchini kutoka 52,633 mwaka 2015 hadi viwanda 61,110 mwaka 2020.
Viwanda vipya vilivyojengwa Katika Serikali ya Magufuli vimeisaidia kuifanya nchi kujitosheleza kwa baadhi ya bidhaa, ikiwemo saruji, nondo na bati. Aidha, viwanda vipya vimezalisha ajira 482,601.
Serikali ya Magufuli imeendelea kuweka mkazo kwenye sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji. Kama inavyofahamika, sekta hii bado ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi Inachangia takriban asilimia 25 ya fedha za kigeni, asilimia 30 ya Pato la Taifa, asilimia 65 ya malighafi za viwandani, asilimia 70 ya ajira zote nchini na asilimia 100 ya mahitaji yetu ya chakula.
Hivyo basi, Serikali ya Magufuli imeongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo (mbegu bora, mbolea, viatilifu, matrekta), imeongeza uzalishaji wa miche ya mazao ya kimkakati, imejenga na kukarabati skimu za umwagiliaji, vihenge vya kuhifadhi mazao, imetafuta masoko na kuviimarisha Vyama vya Ushirika.
Serikali ya Magufuli imeongeza maeneo ya ufugaji kutoka hekta milioni 1.4 mwaka 2015 hadi hekta milioni 5 mwaka 2020 na hivyo kusaidia kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Serikali ya Magufuli imejenga pia majosho mapya 104; imeongeza idadi ya ng’ombe waliohamilishwa kutoka 105,000 mwaka 2015 hadi 514,700 mwaka 2020, imetoa chanjo ya mifugo na kusambaza dawa za kuogeshea mifugo.
Serikali ya Magufuli imeimarisha pia ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi kwa kuanzisha Kanda Kuu tatu: Ziwa Victoria, Tanganyika na Pwani; pamoja na kudhibiti matumizi ya zana haramu.
Serikali ya Magufuli imehamasisha na kufanikiwa kuongeza idadi wafugaji samaki kutoka 18,843 mwaka 2015 hadi 26,474 mwaka 2020; imeongeza idadi ya mabwawa kutoka 22,545 hadi 26,445; vizimba vya kufugia samaki (fish cages) kutoka 109 hadi 431; na uzalishaji wa vifaranga kutoka 8,090,000 hadi 14,531,487.
Sambamba na hayo, mwaka 2017, Serikali ya Magufuli ilizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP – II) wenye malengo wa kukifanya kilimo chetu kuwa cha kisasa, cha kibiashara na chenye tija.
Serikali ya Magufuli imeiongezea mtaji Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) wa shilingi bilioni 208 kupitia mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Serikali ya Magufuli pia imeipatia TADB Dola za Marekani milioni 25.0 (sawa na shilingi bilioni 57.8) ili kuendesha Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) wenye lengo la kuchagiza mabenki na taasisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo kwa wakulima wadogo na makampuni madogo na ya kati ya kilimo (SMEs).
Hii ina maana kuwa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali ya Magufuli imeipa TADB shilingi bilioni 324.8 na hivyo kuiwezesha Benki hiyo kutoa mikopo ya moja kwa moja kwa wakulima, wafugaji na wavuvi yenye thamani ya shilingi bilioni 166.9 kwa riba nafuu.
Katika kipindi cha Miaka Mitano Serikali ya Magufuli Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 15,528,820 mwaka 2015/2016 hadi tani 16,891,974 mwaka 2018/2019. Mahitaji yetu ya chakula kwa mwaka ni chini ya tani milioni 14. Kwa upande wa mazao ya biashara, uzalishaji umeongezeka kutoka tani 796,502 hadi tani 1,144,1631
Katika kipindi cha Serikali ya Magufuli, kwenye uvuvi, sangara kwenye Ziwa Victoria wameongezeka kutoka tani 417,936 mwaka 2016 hadi tani 816,964 mwaka 2020, na urefu wa sangara umeongezeka kutoka wastani wa sentimeta 16 hadi sentimeta 25.2.
Vilevile, Katika kipindi cha Serikali ya Magufuli, mauzo ya samaki wetu nje ya nchi yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 379 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 692 mwaka 2019.
Ushindi wa kishindo kwa Magufuli
Ushindi wa kishindo kwa CCM
Tukutane Oktoba 28, 2020.