Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
Na Debora C. Kiyuga ✍🏽
Miaka Mitano ya Magufuli Serikali imeimarisha uhusiano na ushirikiano na Mataifa ya nje pamoja na taasisi za kimataifa. Hii ndiyo sababu Serikali iliweza kupokea viongozi wa Nchi na Taasisi mbalimbali za kimataifa, ikiwemo Vietnam, India, Uturuki, Afrika Kusini, DRC, Ethiopia, Misri, Rwanda, Zambia, Zimbabwe, Uganda, IMF, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, IFAD na kadhalika.
Miaka mitano ya Magufuli, Serikali imefungua Balozi mpya 8 (Algeria, Cuba, Israel, Korea, Qatar, Namibia, Sudan na Uturuki) na nchi mbili za Ethiopia na Poland pia zimefungua Balozi zao hapa nchini.
Miaka mitano ya Magufuli Serikali imeendelea kushiriki katika shughuli na mipango mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo ulinzi wa amani, ambapo kwa sasa Serikali ina askari wapatao 2,303 katika nchi za DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Lebanon, Sudan na Sudan Kusini.
Miaka mitano ya Magufuli Tanzania imeaminiwa kuongoza Jumuiya mbili za kikanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzia 2016 hadi 2017 na pia kuongoza Jumuiya ya SADC kuanzia Agosti 2019 hadi mwezi Agosti 2020 yenye jumla ya nchi 16.
Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Afrika Kusini, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Angola, Lesotho, DRC, Visiwa vya Madagascar, Comoro na kadhalika zinazokadiriwa kuwa na takribani watu milioni 300 na moja ya mafanikio ambayo Tanzania iliyapata katika kuongoza Taasisi hizi, ni kuzishawishi Nchi Wanachama kuridhia lugha ya Kiswahili kutumika kwenye Taasisi hizo.
Miaka mitano ya Magufuli, biashara ya Tanzania, katika nchi za nje imeongezeka kutoka shilingi trilioni 11.5 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi trilioni 16.6 mwaka 2018/2019.
Miaka mitano ya Magufuli, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwenye masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mfano, kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Dola za Marekani milioni 288.04.
Miaka mitano ya Magufuli Kuhusu uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania kimesajili miradi mipya 1,307 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 14.607, zaidi ya shilingi trilioni 30, na itakapokamilika itatoa ajira 183,503.
Miaka mitano ya Magufuli, Sekta ya utalii imeimarika jambo ambalo limepelekea idadi ya watalii na mapato ya nchi kuongezeka. Kwa mfano, mwaka 2019 tulipokea watalii 1,510,151 kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015. Aidha, mapato yaliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019.
28 Oktoba, 2020 hima tukachague Maendeleo, Tukachague Chama Cha Mapinduzi na tukamchague Rais Dkt John Pombe Magufuli.