BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Na Bwanku M Bwanku
Wakati Rais Dkt John Pombe Magufuli anaingia madarakani Novemba, 2015 na toka nchi yetu ipate uhuru kutoka kwa Mkoloni Mwingereza mwaka 1961, nchi ya Tanzania ilikuwa na jumla ya vijiji 2018 tu vyenye umeme kati ya vijiji 12,268 vya nchi nzima ya Tanzania. Kuingia madarakani tu kwa Rais Magufuli kulifanya maajabu yaliyoshindikana miaka kwa miaka kwenye sekta ya umeme kwa kupeleka umeme mpaka sasa kwenye vijiji vipya 7708 na hivyo kufanya vijiji vyenye umeme Tanzania kufika 9726.
Fikiria kwa miaka mitano tu Rais Magufuli amedouble mara 3 zaidi vijiji vyenye umeme kutoka vijiji 2018 toka tupate uhuru mpaka vijiji 9726 na hivyo kuifanya Tanzania kushika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kupeleka sana umeme vijijini na hivyo kuipiku Afrika Kusini kwa kufikisha Umeme kwa asilimia 85 mwaka huu 2020 kutoka asilimia 35 tu ya watu wenye umeme mwaka 2015.
Ongeza hapo hapo uamuzi wa serikali kupunguza gharama ya kuwaunganishia Watanzania umeme kutoka Tshs 177,000 mwaka 2015 mpaka Tshs 27,000 tu sasahivi. Ongeza uamuzi wa Serikali yake kutekeleza ujenzi wa Bwawa kubwa la tatu Afrika la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (Stieglers Gorge) ambalo likishakamalika litazalisha Megawati 2,115 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi chache Barani Afrika zenye umeme wa kutosheleza mpaka kuwa na ziada, suala litakaloondoa na kumaliza kabisa stori za mgawo wa umeme na abunuasi zake za kukatikakatika.
Mpaka kufikia miaka miwili ijayo nchi ya Tanzania itafikisha umeme kwenye Vijiji vyote 2542 vilivyobaki kwa sababu mpaka hapa tunapoongea serikali iliyo chini ya Dkt John Pombe Magufuli imeshalipa takriban bilioni 851 kwa Tanesco kupitia mradi wa REA ili kupeleka umeme kwenye vijiji vyote vilivyobaki na hivyo kufanya vijiji vyote vya Tanzania kuwa na umeme na hivyo kuifanya Tanzania kuwa moja ya mataifa machache sana duniani kupeleka umeme kwa watu wote.
Kasi hii kubwa ya maajabu ya Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt John Magufuli kupeleka umeme kwa wote inapita mpaka maoteo ya Benki ya Dunia (WB) ambayo yalikadiria sera ya umeme kwa wote kufikiwa karne ya 22 kwenye mwaka wa 2101 lakini kwa kasi hii kubwa ya kupeleka umeme itafanya Tanzania kufika kwenye maoteo ya Benki ya Dunia kabla hata ya muda wake kwa takriban miaka 75 ijayo.
Watanzania wote Oktoba 28, asubuhi na mapema tusifanye makosa wala ajizi, twende tukampe kura za ndio na za kishindo Dkt John Pombe Magufuli ili kazi hii iliyotukuka iendelee👍🏿