Ulitumia tiba gani mkuu?Asante ni Habayu na Dr. Love kwa mawazo yenu. Mimi nilishapona. Miaka mitatu sasa imepita toka nilete uzi huu.
Niliwahi kuwa na tatizo kama hilo three years ago .
Sababu nilikuwa nafanya mazoezi ya kukimbia kila wakati.
Kuna dawa zile za kuchua nilikuwa ninapaka kwenye kisigino kila baada ya kuoga bila kusugua .
Nilitumia kwa wiki kama moja hivi vikaacha kuuma .
Saivi naendelea mazoezi kama kawa tena Masafa marefu bila kuuma.
Jaribu zile dawa za kuchua may be utapona
mkuu hospitali ipi ulienda na kama hutajali naweza kumjua dokta jina lakeSalamu wadau,
Najua ni muda umepita ila nina maarifa kidogo kuhusu haya maumivu ya kisigino kwani nami niliwahi kupata tatizo hili na nikafanikiwa kupata tiba. Nilikuwa na maumivu yanayofanana na mtoa taarifa ya awali kuwa kisigino kinauma sana muda tu ninapoamka toka kitandani (asubuhi) na maada ya shughuli chache (being busy) hayo maumivu yanatoweka ila pindi ukitulia kwa muda unayahisi yanarejea tena.
Nilionana na daktari wa mifupa akashauri kwanza nikapige picha (x-ray) ambayo ilionyesha kuwa sikuwa na athari zozote katika mifupa ya kisigino. Akanambia kama ni hivyo basi nitakuwa na tatizo la msuli kamba. Alimeleza kuwa huu ni msuli unaopita katika kisigino ukitokea katika kidole kikuu cha mguu na wakati fulani inatokea huu msuli unabanwa na nyama za kisigino hasa kutokana na kuongezeka kwa uzito au kuumia mchezoni. Na akanipatia tiba ya sindano aliyoichoma palepale katika eneo la jeraha na nashukura sasa ni zaidi ya miezi sita lile tatizo halijarejea.
Mkuu kama bado upo humu,tunaomba mrejesho tiba gani ilikusaidia.Wadau nawaombeni msaada, kisigino changu cha mguu wa kushoto kinaniuma sana utafikiri labda kuna msumari umeingia, nimewaona wataalamu wengine wakasema huenda ni uzito nipunguze uzito. Nimefanya zoezi na kupunguza uzito karibia kilo tano lakini bado tu. Kisigino kinaniuma hasa wakati ninaamka asubuhi, ila nikiwa busy kinaacha, na nikiwa iddle tu kwa muda kama nikiwatch movies nusu saa tu tayari kinaanza tena! Wakuu naomba msaada wenu!!
Duh hadi mguu una kidney kumbeLazma utakua na matatizo cheki mchoro
View attachment 323952
Uliponaje maana mimi imenianza jana naumia sanaTatizo linaweza kuw limesababishwa na aina ya viatu unavyo pendelea kuvaa
Jaribu kuvaa viatu vilaini (visivyokuwa na visigino vigumu)
Ukiamka asbh, wakati unashuka kitandani nyayuka na vidole vya miguu, tembea navyo km dk mbili hv ndo ukanyage na unyayo wote.
Nilishakuwa na shida km hyo lkn kwa sasa haipo tena
Angalia kiatu unachovaa...Uliponaje maana mimi imenianza jana naumia sana
Juzi nilivaa sandozo alafu mguu wa kushoto ndo unauma kwenye kisiginoAngalia kiatu unachovaa...
Mara nyingi kisigino cha kiatu kikiwa kigumu pia ni tatizo
Asante alafu unauma mguu wa kushoto kwenye kisiginoPamoja na kutumia dawa, acha kabisa soda zote juisi zote na sukari.
Pole
Fanya hicho nimekuambia tu utanikumbuka baadaeAsante alafu unauma mguu wa kushoto kwenye kisigino
Sijakuelewa madam embu nielezee tenaFanya hicho nimekuambia tu utanikumbuka baadae