Kisimbuzi siyo King'amuzi

Kisimbuzi siyo King'amuzi

Megawatt B

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2011
Posts
259
Reaction score
69
Jamani, inasikitisha kuona kwamba bado tunaendelea kupotosha jina halisi na lugha fasaha ya kiswahil kwa hiki chombo kinachoitwa Decoder kwa kiingereza. Decoder kwa kiswahili fasaha ni KISIMBUZI na siyo KING'AMUZI. Na huu mfumo kwa kiingereza tunaouita DIGITAL kwa kiswahili fasaha ni DIGITI na siyo DIGITALI. Watanzania tunahitaji kukienzi lugha yetu, tusije haribu kama tulivyoharibu FISIDI/UFISIDI tukaita FISADI/UFISADI.

Kidumu na kiendelee kiswahili!
 
Ni bora ungeonyesha mamlaka au kamusi kuthibitisha unalosema ili na mimi nipate kukubali - maana kwa sasa naamini maneno yalivyotumika ndio kiswahili fasaha.
 
Jamani, inasikitisha kuona kwamba bado tunaendelea kupotosha jina halisi na lugha fasaha ya kiswahil kwa hiki chombo kinachoitwa Decoder kwa kiingereza. Decoder kwa kiswahili fasaha ni KISIMBUZI na siyo KING'AMUZI. Na huu mfumo kwa kiingereza tunaouita DIGITAL kwa kiswahili fasaha ni DIGITI na siyo DIGITALI. Watanzania tunahitaji kukienzi lugha yetu, tusije haribu kama tulivyoharibu FISIDI/UFISIDI tukaita FISADI/UFISADI.

Kidumu na kiendelee kiswahili!

Ni nani anayeamua kuwa neno fulani ndiyo na hili sio? Mimi nilidhani watu wanatakiwa wazungumze na kutokana na wanachozungumza, mamlaka ndio ziamue ufasaha hasa ni upi.

Baraza la Kiswahili linafanya kazi ya kusahihisha makosa kila siku, sijui wanataka watu wazungumze kama kwenye kitabu?
 
Mbona Antena au Aerial hawakuitafutia jina fasihi katika misamiati ya kiswahili au vitu vingine kama Coffin, Conteiner na Mobile
 
Back
Top Bottom