Kisiwa cha Toten kwenye bandari ya Tanga

Kisiwa cha Toten kwenye bandari ya Tanga

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
3,763
Reaction score
700
Kisiwa cha Toten ni kisiwa kimojawapo cha Tanzania ambacho kinapatikana katika hori ya Tanga kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi. Jina latokana katika Kijerumani "Toteninsel" na kumaanisha "Kisiwa cha Wafu". Wajerumani walitumia jina hili walipofanya Tanga kuwa bandari muhimu ya koloni yao ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sabubu kulikuwa na makaburi mengi kisiwani. Waingereza walipochukua utawala kutoka kwa Wajerumani walikiita "Toten Island" wakichukua "Toten" kama jina hawakutafsiri maana yake.

Kisiwa kina eneo la takriban hektari 16. Kisiwa kinasemekana kuwa na umbo la tanga la jahazi na hapo ni asili ya jina la mji wa Tanga.

Kuna magofu ya msikiti ya karne ya 17 na makaburi ya karne za 18 na 19. Vipande vya vyungu vimepatikana pia ambavyo vyote ni dalili ya kwamba kisiwa hiki kilikaliwa na watu walioondoka baadaye
300px-Tanga_aerial_view.JPG
 
Back
Top Bottom