SoC02 Kisiwa kikubwa cha Taka za plastic katika bahari ya Pasifiki

SoC02 Kisiwa kikubwa cha Taka za plastic katika bahari ya Pasifiki

Stories of Change - 2022 Competition

Blue Marble

Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
25
Reaction score
16
Ukisikia kisiwa basi wote tunafahamu kuwa ni sehemu ya nchi kavu iliyozungukwa na maji. La hasha sio hivyo. Plastc Pacific Garbage Patch ni kisiwa kilichojitengeneza kutokana na kurundamana kwa Taka hasa za plastiki. Kisiwa hiki kinajumuisha taka nyingi za magharibi mwa pwani nchi ya Japani na taka nyingi za Kaskazini Karibu na nchi ya Marekani kwenye Jimbo la Hawaii na Calfonia.

IMG_20220819_162336.jpg

Muonekano wa visiwa vya taka kwenye picha za satelaite — Picha kwa hisani ya mtandao

Taka hizi huunganishwa na ukanda inaoitwa subtropical convergence zone. Watu wajiografia wanafahamu haya mambo, kiasi Cha taka kinacholundamana kwenye The Great Plastic Pacific patch kinatokana na taka zisizooza ambazo nyingi ni plastiki. Chini ya bahari katika kisiwa hiki nako Kuna mlima mkubwa wa taka na watalaamu wa Bahari na wanamazingira hivi karibuni wamegundua asilimia 70 ya taka Zilizopo kwenye kisiwa taka hiki huzama chini ya bahari, wataalamu hawa waligundua kisiwa baada ya bwana Charles Moore aliyekuwa kwenye mashindano ya boti kutoka Calfonia kwenda Hawaii, ndipo alipoona taka nyingi za plastiki zilizotengeneza Kisiwa na waligundua baada ya meli yao Kuzungukwa na mamilioni ya vipande vya plastiki.

IMG_20220819_162346.jpg

Takaza plastiki zikielea chini ya bahari — Picha kwa hisani ya mtandao
Asilimia 54 ya taka zinazopatikana kwenye Pacific Garbage Patch zinatoka kaskazini mwa nchi ya Marekani na Kusini mwa nchi ya Japani, asilimia 20 ya taka zinatoka kwenye boti, shughuli za usafirishaji wa mafuta kwenye pwani Ya bahari na meli kubwa za kusafiri a mizigo ambazo hutupa taka baharini au mizigo kuachwa bahati mbaya.

Karibia tani 700,5000 za taka ni nyavu za kuvulia samaki na taka nyingine kama computa na taka nyingine za plastiki. Na taka hizi zimekuwa hatari kwa viumbe wa Bahari. Mfano kasa na samaki wanaochanganya baadhi ya taka huona Kama chakula Chao, hivyo hula na kufa na wengine kufungwa na baadhi ya taka Kama nyavu na mwisho wao huwa ni kifo kitu ambacho kinatia huruma kwa viumbe hawa.

IMG_20220819_162355.jpg

Kasa akiwa amenasa kwenye nyazu zilizotelekezwa baharini — Picha kwa hisani ya mtandao
Ukiachana na madhara haya kwao, tafiti zinaonesha Kuwa samaki wengi tayari wanavimelea vya plastiki ambayo ni rahisi kwa binadamu kumuathiri kupitia mlo wa samaki, ambao wengi wetu hapa ni wadau wa huyu kitoweo.Madhara ya plastiki kwenye mwili binadamu ni mengi sana. Kama saratani, kuharibu mfumo wa ukuaji kwa watoto nk.
IMG_20220819_162401.jpg

Picha ikionyesha samaki akinasuliwa kutoka kwenye nyavu na mwanamaji (Divers)
Imekuwa vigumu kusafisha taka hizi kutokana na umbali wa kisiwa hicho kutoka kwenye fukwe za nchi zinazopatikana eneo hilo. Mgunduzi wa kisiwa hicho bwana Charles Moore alisema kusafisha kisiwa hicho kunaweza kufilisi nchi kutokana na gharama kubwa zitakazo tumika.

Wataalamu wa Bahari na mazingira walifanya utafiti na kuona zitahitajika meli 67 kwa mwaka kusafisha asilimia moja ya sehemu ya kaskazini ya plastiki Garbage Patch hiyo.. ina maana haitawezekana kabisa kusafisha eneo hilo zaidi ya kuzuia utupaji wa taka hizo.

Wanasayansi na watembezi wamekubaliana kuwa kupunguza na kuondoa matumizi ya plastiki na kuongeza kutumia bidhaa zinazo tumia vifungashio vyenye kuoza na kupotea kabisa baada ya matumizi ndio suluhisho la kuondoa kisiwa hiki kilichojitengeneza kutokana mkusanyiko wa malundo ya taka za plastiki.

Maandishi haya ni kwa hisani ya mtandao.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom