Katika hatua za mwanzo, vipele katika sehemu za
uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya
maambukizi ambavyo baadaye hupotea
vyenyewe.
Kama ugonjwa hautatibiwa, maambukizi huendelea kwa miaka, yakishambulia mifupa, ubongo na moyo na kusababisha madhara mengine yanayotokana na matatizo katika mfumo wa fahamu kama vile homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Kaswende wakati wa ujauzito unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni, kama vile kusababisha kutoumbika vizuri (deformity) na kifo. Wanawake wengi wajawazito katika nchi zilizoendelea huchunguzwa kwa uwepo wa ugonjwa huu katika majuma ya kwanza ya mimba ili kutibu ugonjwa kabla kitoto hakijaathirika. Siku hizi kaswende inaweza kutibika kwa urahisi
fulani kwa penicillin.