Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Kisulisuli niache
Kisulisuli niache, Niache usinivute
Na sitaki nikufiche, Baadae unisute
Hao watu ni vicheche, Usinifanye nijute
*Kisulisuli niache* ,*Hao nawajua Mimi*
Walishindwa kujitunza, Kuheshimu miili yao
Ujana ukawaponza, Na wakakosa upeo
Sasa wamekuwa funza, Watafutao makao
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Heri kumuoa punda, Abebe mizigo yangu
Kuliko kuoa ganda, Walilotupa wenzangu
Hakuna atayependa, Eti chetu kiwe changu
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Kisulisuli wakumbushe, Ndoa sio makalio
Wala wasijibebishe, Na kutaka wenye vyeo
Wambie wasitutishe, Janja haijaanza leo
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Wakiwa makanisani, Kama kuku chini ya mbawa
Wanaporudi nyumbani, Zaidi ya popobawa
Kuoa hatutamani, Punguzeni kuwa chawa
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Kufunga ndoa hiyari, Moyo unaporidhia
Kama hatuko tayari, Mtaishia kulia
Mlijiona sukari, Cheki mnavyojutia
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Ukiwa msichana, Maringo ni kama yote
Majibu yaso maana, Wanaume si chochote
Kutwa kushauriana, Eti ndoa si lolote
Wakishajaa laana, Wanaangaika kote
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Wanaongoza kuroga, Kwa limbwata tuwe bwege
Kutufanya maboga, Kama kuku watufuge
Kisha wakapige soga, Kwa madawa watutege
Hawana hata uoga, Hao ndio vivuruge
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Wasumbua wachungaji, Wazazi na viongozi
Eti haki wazihitaji, Miili ikiwa wazi
Heshima ndo mtaji, Na ndoa ni kama vazi
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Mlioko kwenye ndoa, Msijione kama keki
Mkaanza kusumbua, Waume kutudhihaki
Na kaeni mkijua, Mfupa si mshikaki
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Najua si kupenda kwenu, Ila ndo mjitambue
Tunzeni miili yenu, Someni mjiinue
Lindeni kilicho chenu, Hatua mjipigie
Msiishi kwa fununu, Badae mtusumbue
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
*Ujumbe*
Kisulisuli si dawa ya ndoa, bali tuwafundishe vijana maadili,kuwasisitiza kuwajibika na kuwaandaa kwaajili ya ndoa, Kisha tuwakumbe kuwa ndoa si rahisi kama wanavyofikiria.
Kisulisuli niache, Niache usinivute
Na sitaki nikufiche, Baadae unisute
Hao watu ni vicheche, Usinifanye nijute
*Kisulisuli niache* ,*Hao nawajua Mimi*
Walishindwa kujitunza, Kuheshimu miili yao
Ujana ukawaponza, Na wakakosa upeo
Sasa wamekuwa funza, Watafutao makao
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Heri kumuoa punda, Abebe mizigo yangu
Kuliko kuoa ganda, Walilotupa wenzangu
Hakuna atayependa, Eti chetu kiwe changu
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Kisulisuli wakumbushe, Ndoa sio makalio
Wala wasijibebishe, Na kutaka wenye vyeo
Wambie wasitutishe, Janja haijaanza leo
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Wakiwa makanisani, Kama kuku chini ya mbawa
Wanaporudi nyumbani, Zaidi ya popobawa
Kuoa hatutamani, Punguzeni kuwa chawa
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Kufunga ndoa hiyari, Moyo unaporidhia
Kama hatuko tayari, Mtaishia kulia
Mlijiona sukari, Cheki mnavyojutia
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Ukiwa msichana, Maringo ni kama yote
Majibu yaso maana, Wanaume si chochote
Kutwa kushauriana, Eti ndoa si lolote
Wakishajaa laana, Wanaangaika kote
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Wanaongoza kuroga, Kwa limbwata tuwe bwege
Kutufanya maboga, Kama kuku watufuge
Kisha wakapige soga, Kwa madawa watutege
Hawana hata uoga, Hao ndio vivuruge
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Wasumbua wachungaji, Wazazi na viongozi
Eti haki wazihitaji, Miili ikiwa wazi
Heshima ndo mtaji, Na ndoa ni kama vazi
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Mlioko kwenye ndoa, Msijione kama keki
Mkaanza kusumbua, Waume kutudhihaki
Na kaeni mkijua, Mfupa si mshikaki
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
Najua si kupenda kwenu, Ila ndo mjitambue
Tunzeni miili yenu, Someni mjiinue
Lindeni kilicho chenu, Hatua mjipigie
Msiishi kwa fununu, Badae mtusumbue
*Kisulisuli niache*, *Hao nawajua mie*
*Ujumbe*
Kisulisuli si dawa ya ndoa, bali tuwafundishe vijana maadili,kuwasisitiza kuwajibika na kuwaandaa kwaajili ya ndoa, Kisha tuwakumbe kuwa ndoa si rahisi kama wanavyofikiria.