Kisulisuli niache...

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Copy & Paste

*Kisulisuli niache*

Kisulisuli niache
Niache usinivute
Na sitaki nikufiche
Baadae unisute
Hao watu ni vicheche
Usinifanye nijute
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua Mimi*

Walishindwa kujitunza
Kuheshim mili yao
Ujana ukawaponza
Na wakakosa upeo
Sasa wamekua funza
Watafutao makao
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Heri kumuoa punda
Abebe mizigo yangu
Kuliko kuoa ganda
Walilotupa wenzangu
Hakuna atayependa
Eti chetu kiwe changu
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Kisulisuli wakumbushe
Ndoa sio makalio
Wala wasijibebishe
Na kutaka wenye vyeo
Wambie wasitutishe
Janja haijaanza Leo
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Wakiwa makanisani
Kama kuku chini ya mbawa
Wanaporudi nyumbani
Zaidi ya popobawa
Kuoa hatutamani
Punguzeni kuwa chawa
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Kufunga ndoa hiyari
Moyo unaporidhia
Kama hatuko tayari
Mtaishia kulia
Mlijiona sukari
Cheki mnavyojutia
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Ukiwa msichana
Maringo ni Kama yote
Majibu yaso maana
Wanaume si chochote
Kutwa kushauliana
Eti ndoa si lolote
Wakishajaa laana
Wanaangaika kote
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Wanaongoza kuroga
Kwa limbwata tuwe bwege
Kutufanya maboga
Kama kuku watufuge
Kisha wakapige soga
Kwa madawa watutege
Hawana hata uoga
Hao ndio vivuruge
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Wasumbua wachungaji
Wazazi na viongozi
Eti haki wazihitaji
Miili ikiwa wazi
Heshima ndo mtaji
Na ndoa ni Kama vazi
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Mlioko kwenye ndoa
Sijione kama keki
Mkaanza kusumbua
Waume kutudhihaki
Na kaeni mkijua
Mfupa si mshikaki
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

Najua si kupenda kwenu
Ila ndo mjitambue
Tunzeni miili yenu
Someni mjiinue
Lindeni kilicho chenu
Hatua mjipigie
Msiishi kwa fununu
Badae mtusumbue
*Kisulisuli niache*
*Hao nawajua mie*

*Ujumbe*
Kisulisuli si dawa ya ndoa, bali tuwafundishe vijana maadili,kuwasisitiza kuwajibika na kuwaandaa kwaajili ya ndoa, Kisha tuwakumbe kuwa ndoa si rahisi Kama wanavyofikilia.
 
ila kiswahili ni somo gumu mimi nilifeli big up kwa uandishi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…