Kisunzua

Kisunzua

kwanza wewe una umri gani?
na hivyo visunzua vinakutokea maeneo gani ya mwili?
 
kwani kisunzua ni nini au ugonjwa gani?...madaktari tupeni jina la kitaalamu au la kiswahili fasaha...lugha hizi jamani wengine zinatupa tabu sana watu wa bara sie.
 
Kuna mafuta flani yanauzwa elfu35 yanatibu safi sana ila cha ajabu akiacha yale mafuta kama mwezi ivi vinarudi. Kuna best furendi in need nlimnunulia akawa poa. Mafuta yakaisha vikarudi.
 
Ni ipi dawa ambayo inatibu visunzua na nini chanzo cha huu ugonjwa

Kama kisunzua kimekutoka sehemu ya kawaida nenda pharmacy nunua caustic pencil na mafuta ya mgando (vaseline) upake vaseline kuzunguka kisunzua kisha chovya ile caustic pencil yako kwenye maji na uigusishe kwenye kisunzua, kuwa mwangalifu usiungue ndomana inatakiwa upake mafuta kuzunguka sunzua. Fanya hivyo sehemu zote zenye visunzua na vitapona vyote.
Pia hospitali huwa wanavikata
 
Ina muda gani na ipo sehemu gani ya mwili?

kwani kisunzua ni nini au ugonjwa gani?...madaktari tupeni jina la kitaalamu au la kiswahili fasaha...lugha hizi jamani wengine zinatupa tabu sana watu wa bara sie.

Ndio nini kisunzua?

Mbona hawajibu kisunzua ni nini?

Kisunzua au Masundosundo
[h=2]Ugonjwa wa Masundosundo mwilini na sehemu za siri (Genital & Skin Warts)[/h]

Ugonjwa
kwa kitaalamu vinaitwa human papillom virus HPV,

Vinaambukizwa
kwa mgusano wa damu au wa majimaji kutoka kwa mtu mwenye navyo hadi mwingine, hivyo kupelekea sababu mojawapo ya kuambukiza hivi vinyama kuwa ni ngono zembe.

Nasikia hakuna dawa
ila mwili wenyewe unaweza kuviondoa vyenyewe na kupotea vyenyewe kabisa au huweza kusambaa sehemu mbali mbali za mwili na kuwa tatizo kubwa.

Hatari yake
zaidi huweza leta kansa za aina mbalimbali kwa wanawake na wanaume, sababu hukwenda kubadilisha seli za mwili embu fikiria vikiota ndani ya mwili kwa ndani, basi tena ndio kansa tayari .

Chanjo ipo kwa ambao hajapata ugonjwa huo na kwa watoto wenye umri wa miaka 10 hadi 12, sijui hiyo chanjo kwa hapa TANZANIA au Afrika mashariki ipo?!

Kuhusu Tiba ya hivi vidude kwa njia ya asilia au namna nyingine yoyote; fuatilia mjadala huu...

hpv1.gif
6056155_f260.jpg
 
Mkuu Mzizi mkavu HPV ni kweli unatokana na sababu ulizozielezea ila sijui kama hivyo vinyama vinavyotokea kutokana na ugonjwa huo ni sawa na anasemea mleta mada. Kwanza chunjua kwa kiingereza au lugha ya kitaalam kama inavyosemwa inaitwa wat na sio HPV au inatokana nayo kwa sababu ni watu wengi tu wanavyo au waliwahi kupata, je nao walijihusisha na ngono au kugusana na mtu mwenye maanbukizi? Inawezekana ulichokisema ulimaanisha inayotokana na HPV kwa sababu zinafanana, labda mleta mada aeleze vizuri ijulikane ni vinyama gani hivyo, isiwe anadhani ni sunzua kumbe ni HPV uliyoitaja.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu The Intelligent Human papillomavirus (HPV) is a DNA virus ni Mkusanyiko wa Maradhi ya Zinaa ni Virusivinavyotokana ndani ya DNA. Kwa mfano Mtu akisema Ukimwi sio Ugonjwa ila ni mkusanyiko wa maradhi mwilini mwako Upungufu wa kinga mwilini mwako sasa utakapo umw ana maradhi yoyote mwilini ukiwa huna kinga ya huo maradhi ukienda kupimwa unaonekana unao ukimwi. Na ndio hivyo hivyo hiyo (HPV) inatokana na maradhi ya Zinaa kwa ufupi unaweza kutembelea hapa.https://en.wikipedia.org/wiki/Human_papillomavirus
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwepo navyo kwenye vidole ya mkono wa kulia kama 8 hivi ila haviumi, ukikata damu inatoka nyingi halafu kinaota tena. Nikaja kupata ajali nashangaa kabla majeraha yote hayajapona vyenyewe vikaanza kupotea hadi leo hata ukiniambia nikuonye vilikuwepo maeneo gani siwezi.
 
HAPA NAONA WATAALAMU WANASIGANA TUU...VISUNZUA NI WARTS AU HPV?....ANYWAY MLETA MADA INABIDI AELEZEE UGONJWA WAKE NA DALILI YAKE ULIVYO ILI WATU WATIE NENO JUU YA UELEWA WAO WA TATIZO HILO.

NILIBAHATIKA KUKUTANA NA POST YA VISUNZUA KWA FACEBOOK..KULE ALIWEKA PICHA YA VIJINYAMA VIDOGODOGO SANA VINAKUWA VIMEMTOKEA MTU USONI VINAKUWA VYEUSI KAMA SPOTS ILA NI VIJINYAMA...HATA MH. ZITTO Z. KABWE UKIMTAZAMA VIZURI ALIKUWA NAVYO...KWA HIVYO ALIVYOWEKA MZIZIMKAVU NI VIKUBWA SANA NA SIE TULIKUWA TUNAVIITA SUNDOSUNDO.
 
Chukua samang'ombe ukichome afu uikatiemo, kinapona kabisa
 
Huku kwetu zinaotaga kwenye majaluba ya mpunga, ni vimiti fulan hivi vina mimba, unachukua huo mwiba unaochoma afu unauchamo
 
Back
Top Bottom