figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Temeke Lusubilo Mwakabibi na Edward Haule, Wamefikishwa Mahakamani Kisutu asubuhi hii.
Hatua hii imekuja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa siku nne kwa TAKUKURU kumfika Mwakabibi Mahakamani ajibu Mashitaka yanayomkabiri.
Katika ziara yake ya Jumapili 15 Agosti 2021 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hakuridhishwa na gharama za ujenzi wa miradi ukiwemo ujenzi wa barabara za Kijichi-Mwanamtoti yenye urefu wa kilometa 1.8 iliyogharimu Sh bilioni 5.4 na barabara ya Kijichi-Toangoma yenye urefu wa kilometa 3.25 iliyogharimu Sh bilioni 13.5.
Majaliwa aliigiza Takukuru kuwafikisha mahakamani waliohusika na ubadhirifu wa fedha hizo na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke waliohusika kukopa Sh bilioni 19 kwa ajili ya ulipaji fidia ujenzi wa miradi.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Temeke, Donasian Kessy aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni aliyekuwa msimamizi wa miradi hiyo ya DMDP aliyemtaja kwa jina moja tu la Edward, mhandisi wa mradi na waliokuwa wanamshauri Mkurugenzi.
Wakisomewa Mashitaka nitawapa Update Mashitaka Waliyosomewa. Kama namuona akikaa Chumba Kimoja na Mbowe Korokoroni.
MY TAKE:
Wanasiasa Nawaasa tendeni haki, kuna leo na kesho.
======
UPDATES;
=====
Dar es Salaam. Aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi na mratibu wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam( DMDP), Edward Haule wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka.
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi na jopo la mawakili watatu waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Mshanga Mkunde mbele ye hakimu mkazi mwandamizi, Evodia Kyaruzi.
Chanzo Mwanachi Online.
Pia soma:
1). Mkurugenzi TEMEKE naye akamatwe na ahojiwe
2). Wito: ITV isusie kutangaza taarifa zote za Manispaa ya Temeke mpaka pale DED Mwakabibi atakapotimuliwa
3). Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara
4). Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)
5). Waziri Mkuu Majaliwa, aagiza Lusubilo Mwakibibi kufikishwa Mahakamani