Kisutu: Kesi #458 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums, hukumu yapangwa Oktoba 30, 2020

Kisutu: Kesi #458 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums, hukumu yapangwa Oktoba 30, 2020

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) imeendelea leo, 21 SEPT 2020 asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar.
1600673632613.png

Kutoka Kushoto: Wakili Benedict Inshabakaki, Mwanahisa wa Jamii Media Mike Mushi, Wakili Peter Kibatala, Mkurugenzi wa Jamii Forums Maxence Melo na Wakili Jeremia Mtobesya

Katika shtaka la kwanza, Mkurugenzi wa Jamii Forums anatuhumiwa kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kujasajiliwa Tanzania kwa Kikoa cha do-TZ

Katika shtaka la pili la Shauri hili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa Jamii Forums kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums.com waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea katika Benki ya CRDB.

Taarifa zilizotakiwa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Pia ilitakiwa yaondolewe Mabandiko yote yanayohusu Uhalifu uliokuwa unafanywa na maafisa wa CRDB kitu ambacho Polisi wanadai Mkurugenzi huyo aligoma kuwapa.

Hakimu baada ya kusikiliza pande zote, amepanga kutoa hukumu Tarehe 30 Oktoba 2020. Leo Wakili wa Jamhuri alikuwepo Faraj Nguka na Upande wa Utetezi alikuwa Alphonce Nachipyangu.

Kujua kesi ilipotoka, soma: Kesi dhidi ya JamiiForums (namba 458): Maxence Melo na Mike Mushi wajitetea. Inasubiriwa hukumu
 
Hiyo tarehe tutakuwa na raisi mpya
Rais mwanasheria asiependa ujinga, waziri wa katiba na sheria kichaa mmoja hivi wa sheria, waziri wa mapolice Lema na naibu wake Heche mbona patanoga sana tu hii kesi itaisha siku hiyo na kuna jaji atapigwa pingu siku hiyohiyo
 
Huyo hakimu mjanja. Anataka kwanza ajue nani Kawa Rais halafu hukumu itolewe accordingly!

Kama Rais ni Jiwe watuhumiwa watakiona cha moto, kama Rais ni wa UHM (Uhuru, Haki na Maendeleo), hiyo kesi itayeyuka kama siagi!
 
Back
Top Bottom