Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Aprili 09, 2018
Upande wa Jamhuri leo umefika na shahidi wao mwingine ambaye ni Afisa Msimamizi wa mauzo ya rejareja wa OilCom, Usama Mohammed
Hata hivyo, shauri hili limeahirishwa mpaka tarehe Mei 03, 2018 baada ya Hakimu Simba kusema anahitaji muda kutatua tatizo dogo la kisheria alilikumbana nalo wakati anasoma jalada ya shauri hilo
Ikumbukwe Hakimu Simba anasubiriwa kutoa uamuzi mdogo juu ya ushahidi uliochapishwa na kutolewa na upande wa Jamhuri
Ushahidi huo ulipingwa na Mawakili wa Utetezi wakisema ushahidi huo hauwezi kutumika kwa kuwa kuna taratibu za kufuata ili ushahidi wa kuchapishwa uweze kutumika.
Kwa kujua kesi hii ilipotokea rejea hapa; Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa. Hakimu hajamaliza kuandika uamuzi mdogo(ruling)