KISWAHILI AU KIINGELEZA?Ipi ifundishie mashuleni.

KISWAHILI AU KIINGELEZA?Ipi ifundishie mashuleni.

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,126
KUMEKUWEPO NA UBISHANI MKUBWA KUHUSU MATUMIZI YA KIINGELEZA KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA BADALA YA KISWAHILI.

nini maoni yako?

Zingatia
1.kiingeleza kinadaiwa kuchangia matokeo haya mabaya ya sekondari
2.kiingeleza hakieleweki kwa wanafunzi wengi
3.ufaulu wa somo la kiswahili fm 4 ni D kwa wanafunzi wengi.
4.shule ya msingi pia hatufanyi vizuri japo tunatumia kiswahili
5.zamani kiingeleza hakikuwa tatizo kwa wanafunzi na walifanya vizuri sana
6.wapo wanafunzi watanzania waliosoma kozi ya miezi 6 ama 12 na kuelewa lugha za kirusi,kichina,kijerumani na walitumia lugha hizo kufundishiwa na hawakusumbuka.
JE TATIZO NI LUGHA ama TATIZO NI KUWAFANYA WANAFUNZI WAIELEWE LUGHA YOYOTE WANAYOFUNDISHWA?
 
Sidhani kama lugha inachangia at large percentage. ..maana waanze kufundisha kiswahili tu mbona urusi, japan, german wanafundisha kwa lugha zso tu.

Mimi naona tatizo ni weak syllabus na walimu hawajataarishwa ipasavyo
 
Maoni yangu si hoja, zingatia uandishi.
Kiingeleza si lugha, kiingereza ndo kweli.
Kabla ya kusema sana, fikiria uandishi.
Ndo maana tunafeli, kwa sababu ya papara.
 
Tatizo la Kiswahili ni kwamba kuna maneno mengi hakina, kinyume na Kijerumani, Kirusi, Kichina nk. Lugha hizi wamehakikisha kwamba mtu anaweza funzwa somo lolote bila kuchanganya neno la Kingereza kwenye sentensi. Kiswahili tunakipenda, lakini tukiboreshe zaidi kwa kuhakikisha tunaongeza maneno yaliokosekana.
 
KUMEKUWEPO NA UBISHANI MKUBWA KUHUSU MATUMIZI YA KIINGELEZA KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA BADALA YA KISWAHILI.

nini maoni yako?

Zingatia
1.kiingeleza kinadaiwa kuchangia matokeo haya mabaya ya sekondari
2.kiingeleza hakieleweki kwa wanafunzi wengi
3.ufaulu wa somo la kiswahili fm 4 ni D kwa wanafunzi wengi.
4.shule ya msingi pia hatufanyi vizuri japo tunatumia kiswahili
5.zamani kiingeleza hakikuwa tatizo kwa wanafunzi na walifanya vizuri sana
6.wapo wanafunzi watanzania waliosoma kozi ya miezi 6 ama 12 na kuelewa lugha za kirusi,kichina,kijerumani na walitumia lugha hizo kufundishiwa na hawakusumbuka.
JE TATIZO NI LUGHA ama TATIZO NI KUWAFANYA WANAFUNZI WAIELEWE LUGHA YOYOTE WANAYOFUNDISHWA?
h. Hebu mshinga jitahidi kumakinika ili ueleweke basi. Kwenye orodha ya lugha hakuna lugha inayoitwa Kiingeleza. Hebu tusaidie tujue lugha hii huzungumzwa wapi na ilianza kufundishwa lini kwa wanafunzi wa hapa nchini?
 
kiswahili kikitiliwa mkazo kama lugha ya kwanza kwa kufundishia shuleni wanafunzi watafanya vizuri zaidi na ufaulu utakuwa mkubwa
 
English mkuu,waajiri wote wanatumia kiingereza kama lugha ya kiofisi
 
Back
Top Bottom