eti soda ni daso...
eti gari ni dinga au bodi...
petroli ni ngata..
mtu ni mdhi
msichana ni manzi au siste au shore au chile au mshi (m-she), na mhi (m-he)
katia manzi ni flirting
kumnoki msichana ni kumpenda kiasi
cheki badala ya tazama
lapa mtu ni kumdharau au kum-ignore
kugota msee ni "fist bump"
vako ni kaa mauwongo ya msee
msee ni mtu hajazeeka bado, mtu asiye "mzee" ni msee.
pesa ni chapaa
mkalio/------ ni mahaga au rasa
hapana/la huwa zii
mtu mzii ni mtu mkali..
sasa? badala ya habari?...na kujibiwa ni "fiti"
boli ikiishwa na pumz ni vile haina pressure
na pia we, ukiishwa na pumz ni vile umechoka
iza ni kaa kusema pole
mtoi ni mtoto
jo/ngai ni kaa kusema ala!
na hizo ni za kitambo, i'm sure nikienda maruaundi nai ningezipata zingine mob.
ni vile sijafika those sides in too long.
mazee tuliharibu lugha tukiwa watoi, jo!
mi huhisi sitaruhusu mawanawangu wabonge sheng wakiwa hao. sheng ni ujinga tupu, tebu tuiache enyee...