Kiswahili cha Kitchen Party,Send off na Massage hiki hapa

Jimjuls

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
486
Reaction score
168
Maneno haya huwa tunatumia kila wakati hata kwenye kadi zetu za mialiko.
Kitchen Party-sherehe mfundo
Send off- sherehe muago
Massage- kusigwa
Salon- Chega
 
Maneno haya huwa tunatumia kila wakati hata kwenye kadi zetu za mialiko.
Kitchen Party-sherehe mfundo
Send off- sherehe muago
Massage- kusigwa
Salon- Chega

Massage - kusingwa
 
Maneno haya huwa tunatumia kila wakati hata kwenye kadi zetu za mialiko.
Kitchen Party-sherehe mfundo, Send off- sherehe muago, Massage- kusigwa, Salon- Chega

Umesikiliza kipindi cha radio one cha jana, ila na wale nao ikiwa hawajui kitu fulani hawataki kukubali.

Hakuna kitu sherehe muago hicho ni kiswahili gani? Kwanza hatuna utamaduni wa send off kwenye harusi zetu za kiswahili na hata huko kwenu mabara. Haya ni mambo ya kuiga kutoka uzunguni na yameanza kwenye kati ya miaka ya themanini baada ya hali ya kiuchumi ya watu kuwa ina afadhali.

Kitchen party kwa kiswahili hasa ni 'kwenda kufundwa' au kwa wa pwani wataelewa neno 'sherehe ya kapu' kwani hapo ndiyo mashangazi, mabibi na wengine huja na zawadi za biharusi na huku wakiwa na maneno yao ya nasaha kwa biharusi mtarajiwa.
 
Ama kiswahili kinakimbia sana. Massage=kusingwa? Kwa muda mrefu mie nilijua maasage= kukanda
Haya, asanteni waungwana kwa kutujuza

Kwa kweli hata na mimi jana niliposikia tafsiri ya massage kuwa ni kusingwa nilishangaa kidogo, maana najua ni kukandwa. Kusingwa ni kwa liwa (sandalwood au sandali) na kukandwa ndiyo kwa mafuta. Sasa jee kuna watu wanasingwa kwa mafuta tu bila kuhusisha liwa?

Ndiyo mana nikasema hawa wataalamu hawataki kukubali kwamba hawajui huwa wanajisemea tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…