Kiswahili Hakijitoshelezi. Amin hivyo

Joined
Jan 5, 2011
Posts
25
Reaction score
3
Habar wana JF. Ulishawahi kujiuliza sifa za lugha Yoyote Maarufu Duniani? Au Ili lugha iweze kuwa Maarufu, wajua moja ya sifa!? Ntazungumzia KipengEle kimoja tu cha Kujitosheleza Kimsamiati na Maneno. Tuchukulie mfano wa Lugha kama Kiingereza. Wenzetu hawa neno Moja linakuwa na Mbadala wa Maneno mengine ya ziada. Wao huita "Synonyms" Mfano Happy/Joyful/Elated. Sasa basi shughuli inakuja kwenye Upande wa Kiswahili. Kama hata neno moja halipo hiyo synonym itAtoka Wapi!? Hivi ni kweli Lugha yetu inakosa Neno kwa ajili Mtoto wa Mbuzi!? Sasa ukiulizwa synonym ya Mtoto wa Mbuzi sijui itakuwaje kama hata hilo Neno Moja tu lenyewe halipo. Embu tuchangie hapa jamani. Jina halisi kwa kiswahil fasaha kwa ajili ya Mtoto wa Mbuzi kama ilivyo kwa Ndama.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
mbalelo............... huyu ni ndama wa mbuzi ama mtoto wa mbuzi
 
Dah kwanza naomba kutoa sifa ambazo zinatakiwa ili lugha iweze kuwa maarufu ni lazima itimize haya yafuatayo
1. lazima iw na wazungumzaji wengi wazawa na wasiyo wazawa
2. lazima iwe imeenea sehemu kubwa sana (imechukua eneo kubwa kijiografia)
3. lazima itosheleze mahitaji ya sayansi na tknolojia
4. lazima iweze kuandikwa na kusomwa kwa urahisi.
Kutokana na hoja hizo ni wazi kwamba kiswahili kinazo sifa hizo japo kuna mapungufu mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika lugha yoyote ile na kupelekea lugha hiyo kukopa kutoka za nyingine zilizo karibu nayo. Ama kwa upand wa kulinganisha ubora kati ya lugha kiswahili na kiingereza ni wazi kabisa kiswahili ni bora kwa kigezo cha msamiati kwani lugha ya Kiswahili imekopa asilimia 40 ya maneno yake kutoka lugha zingine huku lugha ya kiingereza imekopa asilimia 60 ya msamiati wake kutoka lugha zingine. Hivyo ni wazi lugha ya kiswahili imatumia msamiati wake yaani asilimia 60 na kiingereza kinatumia asilimia 40 tu ya msamiati wake so kiswahili ni bbora bhan
 
Mkuu Wilhard nakuheshimu lakini acha nitofautiane na wewe kwa hoja.
1.Lugha ya Kiingereza ina umri wa miaka karibu 1000. Hata katika umri huo Kiingereza kimekopa maneno kutoka lugha nyingi. Mifano:

a. Kiswahili: Kiingereza[English] kimekopa neno "safari" je, wajua hilo?
b. Kigiriki: maneno ya mengi ya Kiingereza yanayoanza na "photo" yanatoka kwenye Kigiriki. "Graphics" na mengine chungu nzima.
c.Alfabeti za Kiingereza zote zimetolewa katika lugha ya Kigiriki isipokuwa "Q" na "W", kwa sababu Kiingereza kina alfabeti 26 lakini katika alfabeti hizo 24 ni kutoka Kigiriki.

*Jambo la kukumbuka ni kwamba, lugha ni "Dynamic", siyo "Static", yaani lugha hubadilika kulingana na muda na umbali kutoka chanzo. Mfano Tanzania "dhambi" lakini Congo D.R, "zambi".
Jaribu kufanya utafiti kabla ya kuanza kushutumu. Je, wewe unajua Kiingereza kwa kiwango cha Mwingereza mwenyewe?
Mkuu Merick David, asante kwa kumsaidia ndugu yetu!:smile:
"Be bold, and mighty forces will come to your aid"
 
Kiswahili kinajitosheleza kabisa kama lugha nyengine yoyote,mataizo tuliokuwa nayo sisi watanzania kisawahili hatukijui na wengi wa Watanzania kiswahili ni lugha yao ya pili
 
Kiswahili kinajitosheleza kabisa kama lugha nyengine yoyote,mataizo tuliokuwa nayo sisi watanzania kisawahili hatukijui na wengi wa Watanzania kiswahili ni lugha yao ya pili
Haswa, naona mtoa mada ndio ambaye hajitoshelezi. Yaani hajitambui, kwa hiyo bado hajakamilika na badala yake anaisingizia lugha. Kazi anayo!
 
mbalelo............... huyu ni ndama wa mbuzi ama mtoto wa mbuzi

Waja wasojaa wala kujua Kiswahili faradhi ya forodha, kukiiza hasara na halasa. Hawakikidhi hata sudusu ya msamiati sahala, seuze wa tambo la tembo mgida tembo.

Wabeza Kiswahili bila ku ree nyenzo korija ni kama watupa johari kwa utovu wa majadi.
 

Kiingereza mbona ni dhahiri kabisa kwamba hata chenyewe hakijitoshelezi hadi kinaazima hata maneno ya Kiswahili..

Bofya hapa na hapa uone.
 
Hakuna lugha duniani inayojitosheleza bila kukopa maneno toka kwenye lugha nyingine.

Kiswahili ni lugha yenye nguvu, imeweza kuunganisha watu wa afriaka mashariki na kati. Hivyo inaweza kufanya makubwa zaidi ikiwezeshwa na kuendelezwa na wataalam wa lugha.

Tatizo ni kwamba hakuna jitihada za ziada zinazofanywa na serikali kukikuza na kukiendeleza.

Hata wew mtoa mada una-suffer from slavery mentality kwa kuamini english ni bora kuliko kiswahili.. Tazama historia ya kingereza na jinsi serikali yao ilivyo fanya jitihada za kukifikisha kilipo leo hii. Kingereza hakikufika hapa by chance, watu walifanya kazi kukisoma na kukiendeleza usiku na mchana na ndo mana upo leo unapuuza vya kwako na kuamini vya wenzako ndivyo bora. Poor you! You need some mental liberation. And I mean some serious one!
 
Waja wasojaa wala kujua Kiswahili faradhi ya forodha, kukiiza hasara na halasa. Hawakikidhi hata sudusu ya msamiati sahala, seuze wa tambo la tembo mgida tembo.

Wabeza Kiswahili bila ku ree nyenzo korija ni kama watupa johari kwa utovu wa majadi.
Kiranga i cant you broda!
mie nlijua bombastic words wazitumia kwenye kiigereza tu kumbe hata huku kwenye kiswahili umo??
asante sana kwa kunifaanya nipate misamiati 10 mipya.
 
Last edited by a moderator:

Ngoja na mimi nikuulize swali, nipe tafsiri ya maneno haya kwa kiingereza, Baba mdogo na baba mkubwa, mama mdogo na mama mkubwa, na shangazi!

 
Kijakazi una akili sana!
Mfano wako ni mzuri sana:
Acha niongezee mambo machache muhimu kuhusu lugha:
1.Kazi kuu ya lugha ni kuwasiliana sasa iwe Kiingereza kina maneno mengi na visawe chungu nzima, hiyo si hoja!
2. Wazungu hawatofautishi kati ya baba mdogo na mjomba, sisi Waswahili tunawazidi hapo. Wao husema "uncle" tu.
3. Wazungu husema "rice", lakini Waswahili hutofautisha kati ya "mpunga", "wali" na "mchele"

:high5:
 
Huyu Wilhard kaanzisha mada halafu yeye mwenyewe kaingia mitini. Hebu njoo huku sasa tuendelee!
 
Last edited by a moderator:

Shoga angu embu nipe synonym ya maneno kama 'ugali', 'gubu' 'sanda' na kadhalika katika Kiingereza.
 

Agosti hapo namba 3,wazungu mpunga huita paddy, ingawa hata shamba la mpunga huitwa hivyohivyo.
 
Niseme tu ajabu kubwa lugha inayojitosheleza yaani Kiingereza haina neno la HODI. Pili Kiingereza kimezoa na kinaendekea kuzoa manenokibao kutoka Kilatini na Kigiriki.
A critical look is what you need.

 

USA Torch ni Flashlight, Lorry ni Truck, spanner ni wrench.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…