SoC02 Kiswahili kiwe ni ngao Tanzania

SoC02 Kiswahili kiwe ni ngao Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 22, 2022
Posts
7
Reaction score
3
UTANGULIZI
Nifaraja kwangu na Waswahili wote katika mwambao wa Afrika Mashariki hata wale wapenzi wa Kiswahili ambao watasoma andiko hili tena kwa kutumia hicho hicho Kiswahili.kwa sasa Kiswahili hatuwezi kukifasiri kwa ukubwa wake kwani kina ithibati ngingi ambazo zinakipambanua na kukifanya kichapuze midomo ya Wasemaji wote Duniani, hili si kwangu tu hata JAMII FORUMS ambao ni wadau wakubwa wanatetea kiswahili.itoshe kusema 'KISWAHILI KIWE NI NGAO TANZANIA'.

MADHUMUNI
Andiko hili litajikita kuangalia namna ambavyo Tanzania inafaidika kupitia Kiswahili kwa kuangazia mchango wake katika nyanja za Elimu, Uchumi, siasa na Utamaduni ambavyo ndio viini vya dongoo zitakazoelezewa.Pia Andiko hili litaonesha Viongozi mbali mbali vyalivyopania kukikuza Kiswahili kwa kujivuna mbele ya Majukwaa huku wakitetea hoja zenye msimamo kwa kutumia Lugha hii ya uzawa.Dondoo zifuatazo zinaelezea namna Kiswahili kinavyochochea Maendeleo na Kutumika kama ngao Tanzania.

Kiswahili kinadumisha Uhusiano na ushirikiano miongoni mwa Tanzania na nchi nyengine. Katika siku za hivi karibuni kiswahili kimekua ni Lugha muhimu sana kuhusu uhusiano na ushirikiano miongoni mwa nchi nyingi duniani.Hali hii imebainika wakati wa Mkutano wa 39 wa nchi zinazounda umoja wa nchi za kusini mwa Afrika(SADC), wakati huo Kiswahili kilihesabiwa miongoni mwa lugha saba muhimu ambazo zitatumika kuunganisha umoja wa nchi hizo.

Kiswahili kinajitosheleza.Kama tujuavyo kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya watumiaji wake, vivyo hivyo kiswahili kinatosha kwa shughuli zote muhimu ndani na nje ya Tanzania.kuna ithibati ya hili hebu tujikumbushe kipindi cha 'Hayati John Magufuli' kutokana na utoshelevu wa Kiswahili alitumia kama kigezo katika Mahaka na alimpandisha cheo Jaji 'Zafarin Galeba kutokana na kutumia Kiswahili akihoji na kuamua kesi.utoshelevu huo huo ndio uliotumika katika kuendesha mkutano wa 39 na 40 wa nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).

Kiswahili ni Lugha ya kwanza katika mwambao wa Afrika Mashariki.nchi nyingi za Mwambao zinatumia kiswahili katika mambo mbali mbali ikiwemo kufundishia hali inayofanya Kiswahili kiwe Lugha ya kwanza na bora ya nchi hizo.

Tanzania tukiwa nchi mama kwa matumizi ya Kiswahili, mambo haya yangefanyika ili kukikomaza na kukita mizizi na kua ngao bora.

Kutumika katika kutolea Elimu kwa ngazi zote.hapa ni wajibu wa serikali kubadili nafasi ya Lugha ya kufundishia katika ngazi zote za Elimu, yaani masomo yafundishe kwa Lugha ya Kiswahili ukitoa masomo ya Lugha kama kiingereza na kiarabu, kifaransa nk.

HITIMISHO
Ingawa Tanzania ni taifa litokanalo na utawala ambao uliathiri Lugha na mfumo mzima wa maisha, hatuna budi Kiswahili kukitumia kama mataifa mengine yaliyofanikiwa kupitia Lugha zao.

Wenu.Habibu hamadi haji (manji).
Barua pepe.habybuhaji@gmail.com
Mwanafunzi, Chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar (SUZA).
 
Upvote 5
Sawa Kiswahili ni ngao pita na kwangu "Vita ya vijana dhidi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia"
 
Andiko zuri sana kwa naendeleo ya Lugha yetu.
 
..Tudumishe lugha zetu za asili.

..lugha za asili zinachangia kukuza Kiswahili.

..Tusiache kujifunza Kiingereza.

..Kutokana na HISTORIA Kiingereza ndiyo lugha kiunganishi ya dunia.

..Kiingereza ni lugha ya kubadilishana utaalamu na maarifa mbalimbali.

..Wanasayansi wa Kitanzania, Kichina, Kijerumani, na Kibolivia, wakikutana uwezekano mkubwa wataongea Kiingereza.
 
Back
Top Bottom