Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Watu wengi sana utawasikia wanakwambia mimi sijui lugha ya mama ni Kisukuma, sijui Kichaga mara mimi sijui Kihehe woote ni Waongo!
Lugha ya mama Tanzania ni Kiswahili nikimaanisha kwamba Lugha ambayo Mtanzania wa kawaida anaiweza kuiongea na kuiandika kuliko Lugha nyingine yoyote ile, nasema hivi kwa maana zaidi ya 70% ya Watz (Vijana) hata waliozaliwa vijijini ingawaje wanaongea lugha mbili lkn ukiwauliza lugha ambayo wanaweza kuiongea kwa umakini na umahiri mkubwa kati ya Kiswahili na kilugha kingine watakwambia ni Kiswahili lkn ukimuuliza wewe Lugha yako ya kwanza ni ipi atakwambia ni kihehe au Kisumbwa! Hivyo wengi hawaelwei maana ya lugha ya mama ni nini!
Huu ni utafiti uliofanywa na niliofanya pia nilikuwa kwa mfano KLM vijijini huko nakutana na vijana wengi ambao hata hawajawahi kufika Moshi mjini hicho kinachoitwa Kichaga wanakiongea lkn kinawapa shida na ni lazima achanganye na Kiswahili, na ukimuuliza achague Lugha ambayo anaweza kujielezea kwa umakini kabisa hatochagua Hicho kinachoitwa Kichaga bali atachagua Kiswahili!
Na Mikoa yote ni hivyo hivyo, Nilikuwa Usukumani huko Bariadi vijana wote mpaka miaka 25 ingawaje wanaweza kuongea hicho kinachoitwa kisukuma lkn kuna mahali wanakwama na wanaingiza Kiswahili, na ukimwambia achague Lugha ya kukuelezea kitu basi atachagua Kiswahili na wengi humu mtapinga hili nikiwaambia mnielezee kitu kwa Ufasaha mtachagua kwa Kiswahili
Hivyo Lugha Mama ya Tanzani Ni Kiswahili!